Arsenal Bado wapo na Walcot ni kichekesho kwa kweli, Barcelona imemchukua Ousmane Dembele sina uhakika sana na uwezo wake, Man utd bado wana Lingaard ni aibu kubwa ila wanamtaka Perisic (fununu zinadai wanamtaka mahrez), Wakati hayo yote yanatokea, Riyadh Mahrez ana thamani ya Euro 40 tu (naona kama Leicester wanatutania). Ni mchezaji mzuri kabisa asiye na doa lolote la wasiwasi juu ya uwezo wake na ana bei ya kawaida kabisa lakini nani anamtaka?
Nani ambaye hajui uwezo wa Mahrez? Kwanini timu kubwa hazimtaki? Hivi Ousmane dembele na Mahrez nani ambaye tunaweza kusema anaweza kuhimili presha? Je Barcelona hawakumuona Mahrez akipewa tuzo ya mchezaji bora England na Africa? Kwanini watumie Euro 105 kwa dembele wakati kuna fundi wa Euro 40 tu aliyesaidia timu ndogo kabisa kufanya maajabu yaliyofanywa na Garry Birtles akiwa Nottingham Forest mwaka 1978 walipotwaa ubingwa wa ligi mbele ya Liverpool na yale yaliyofanywa na John Baraza mwaka 2009 kwa kuziacha Tusker Fc, Gor Mahia na Fc Leopard kwa kuisaida sofapaka kutwaa ubingwa. Leicester ilikuwa mabegani mwa Mahrez nani hakuona hilo?
Ni mwarabu gani unayemjua wewe mwenye mafanikio makubwa England kama Mahrez? Hivi tukiondoa Zidane kuna mwarabu mwingine ambaye atakumbukwa na wazungu kwenye soka kwa miaka 20 iliyopita?samahani Usinitajie Benzema, wala sitegemei kuniambia Anelka. Hivi kipaji cha Hartem Ben arfa ni cha kuhangaika kama Henry Joseph Shindika ulaya?
Hivi Samir Nasri ni wa kutapatapa kama Lipumba kweli? Kwanini waarabu hawana thaman ulaya? Nahisi Jibu analo Edo Kumwembe aliyewahi kusema kwenye makala zake kuwa waarabu wakorofi sana na wana kiburi.
Ferguson alimkataa Nasri, alimkataa Ben Arfa, Mourinho alimkataa salah, klopp alimruhusu Mohomed Zidan kuondoka, jiulize kwanini? Dimitri Payet ana uwezo wa kucheza klabu yoyote kubwa duniani leo yupo Olympic Marseille akiwa hana mbele wala nyuma. Hili suala la Mahrez limenifanya nikumbuke kizazi cha wana Misri, ambao ulaya pamekuwa kama magogoni kwenye akili za vigogo wa ukawa. Nimewakumbuka sana akina Mohammed Aboutrika, nimemkumbuka jinsi Mido na zaki walivyokuja kama Upepo na Kupotea.
Maandiko matakatifu yanadai kuwa jeshi la Wamisri lililokuwa chini ya farao lilizama bahari ya shamu. Inaonekana kila waarabu wanapovuka ile bahari ya sham hawafanikiwi sana. Sijajua ule mkosi wa Farao kama bado unakula kama usaliti wa Mugabe ulivyotafuna uchumi wa Zimbambwe. Mwarabu pekee anayecheza uwanjan kwa sasa mwenye mafanikio makubwa licha ya kuwa ni mojawapo na mastriker wabovu kwenye macho yangu ni Karim Zidane Benzema. Namwita hivo kwakuwa naamini uwepo wa zidane klabuni hapo unamfanya jamaa azidi kula maisha Mjini Madrid. Wapo wengine kama akina Mehd Benatia lakini kwa kiasi kikubwa hawana majina makubwa wala ufalme kama unavyowazungumzia waafrika ulaya kama Drogba, Eto'o , aubemeyang n.k
Niliwahi kumzungumzia Omary Adbularhman. Huyu ni mchezaji mwenye uwezo zaidi ya Andrey Gomes mara kumi yake.
Wakati Rijkaard anaongezeka kwenye listi ya watu waliomsaidia Lionel Messi akaamua kumpa nafasi baada ya kushauriwa na mwalimu wake bwana Rondell, Ommy anasaidiwa kufikia mafanikio yake, na kocha Winfred Schafer baada ya kumpa nafasi kucheza kikosi cha kwanza akiwa na miaka 16 tu. Messi huyu wa Asia alifunga magoli 6 kwenye michezo 10 na kutengeneza mengine matatu. Msimu wa 2009 aliweka kimyani magoli matano kwenye michezo saba, msimu wa 2010 alifunga magoli 11 kwenye michezo 29 na kutengeneza magoli 8 ikiwa ni msimu wake wa pili.
Mwalimu wa kikosi cha watoto Man city bwana Brian Marwood alimfuata ommy mpaka falme za kiarabu. Alipomkuta aliiomba klabu ya Al ain kumruhusu waondoke nae kwa majaribio ya wiki mbili kwa makubaliano ya kumsajili kabla ya dirisha kufungwa. Alifanya majaribio ambapo klabu ya Man city ilikubali kumpa mkataba. Kama kawaida gundu la waarabu lilimtafuna kama mkosi wa watu wa kaskazin lilivyontafuna Lowassa kule dodoma 2015. shida ya vibali ya kazi pamoja na viwango vya FIFA vya taifa lake havikukidhi kwa yeye kucheza ligi kuu England.
Ommy ametakwa sana na Barcelona. Binafsi nilipomwona niliona kama ndiye mrith halali wa Xavu, cha ajabu Barcelona walimnyenyekea Ivan Rakitic baadae wakamleta Andrei Gomes, kisha Delafeou.
Mwaka 2013 Ommy aliweka rekodi ya kutengeneza magoli 23 kwenye michuano yote ikiwa ni pamoja na kutengeneza magoli 17 kwenye ligi kuu Saudia, pia alitajwa kuwa mtengenzaji magoli bora kwa misimu miwili mfululizo 2013 na 2014. Bado Barca na Man city zimefumba macho. Akiwa na miaka 25 tayari ana mafanikio makubwa ndani ya bara la Asia, kwa aina yake ya uchezaji binafsi bado namwona ni mchezaji bora ndani ya bara la Asia kwa wazawa. Tayari ameisaidia klabu ya Al Ain kubebwa ubingwa wa ligi za kiarabu, ubingwa wa ligi, super cup, kombe la Rais, na ubingwa wa AFC. Ametajwa kama mchezaji bora wa klabu mwaka 2008, na 2009, alitajwa pia kuwa mchezaji bora chipukizi 2009, 2010, mchezaji bora wa mwaka kupitia Al Ahram 2010, mchezaji wa thamani kwenye michuano ya ubingwa wa ligi za kiarabu mwaka 2010, mchezaji bora wa mashabiki kupitia AGL 2012, pia aliwahi kuwa mchezaji bora chipukizi kupitia Al Hadath 2013, na mchezaji bora wa Emirate 2013.
Mchezaji bora wa bara la Asia 2016, mchezaji bora wa ABA ligi kuu zote za Asia 2015, mchezaj bora kupitia GSA, AFC 2016, al haram mchezaji bora 2015/6, mchezaji bora wa Emirate kupitia AGL kwa msimu wa 2014/15/16. Yaani ukiangalia vizuri hizi tuzo anatosha kabisa kuwa mchezaji bora wa kiarabu kwa miaka ya hivi karibuni na ana haki ya kuwa moja ya wachezaji bora wa kiarabu kama atapata nafasi ulaya
Huyu ndiye Messi wa Asiana ndiye mshindi waMars D Or mchezaji bora wa kiarabu mwaka 2015. lakini hata akija ulaya gundu la kaka zake waliomtangulia la kushindwa kupata makazi sahihi na yenye ufalme litamwacha salama kweli?
No comments:
Post a Comment