CHEKA ATUPWA MAGEREZA

Cheka ‘ SMG ’ amehukumiwa miaka mitatu jela katika Mahakama ya mkoani Morogoro. Taarifa zilizotufikia punde zinaeleza Cheka amepatikana na hatia ya kushambulia baada ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake. Pamoja na kifungo cha miaka mitatu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ni hiyo, Said Msuya amemhukumu Cheka kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho. Cheka amepatikana na hatia ya shambulio dhidi ya aliyekuwa meneja wa baa yake, Bahati Kibanda aliyemshambulia Julai 2 , mwaka jana katika Ukumbi wa Vijana Social aliokuwa ameukodi kwa ajili ya kuendesha shughuli za baa zilizokuwa zinasimamiwa na Kibanda. Kutokana na kukutwa na hatia, Cheka amehukumiwa kwenda jela kwa muda huo na imeelezwa tayari ameshapelekwa kwenye gereza mkoani humo.

No comments

Powered by Blogger.