AMBASSADORS OF CHRIST-SHERIA LYRICS

Ambassadors of Christ

Shairi la 1

Zipo Sheria pia amri za barabarani
Zitupasazo kuzitii tukiwa safarini
Kinachoshangaza muda Mwingi
Tunasahau kuwa hizo amri
Zipo kwa usalama wetu
Ndio sababu unawaona Madereva
Wakiendesha kwa kuchungana na Polisi
Mwendo mkali bila kujali chochote
Maisha yake hata Maisha ya Wengine
Pale atapomwona askari kwa mbali
Atajifanya kuzijali amri na sheria
Kusudi ampendezee askari huyo
Ila sio kwamba ajiepushe na ajali

Kiitikio

Hivyo Ndivyo ilivyo sheria ya Mungu
Ipo kwa usalama wetuu
Mungu mwenyewe haimsaidii kwa lolote
Ila ni kwa faiida yetu,
Lakini siku hizi za Mwisho yapo Mafundisho
Yakwamba amri zake Mungu hazifai tena
Usidanganyike ndugu msafiri Mwenzangu
Bila amri ya Mungu hatutafika salama

Shairi la 2

Katika safari hii ya wokovu twahitaji
Mwongozo tuwekwe sawa na jamii ya Mbinguni, kama ni kweli twauthamini wokovu ule,
basi tutazishika amri kwa usafi wetu,
Kama ni kuiba madhara yake twayajua
Je kuziini matunda yako wazi
Usidanganye kumbuka pale ulipodanganya
Na jinsi ulivyokosa aman Moyoni
Jambo hili li wazi kwamba jamii ili yoyote
Huwa na utamaduni pia desturi yake
Kwa hiyo kazi yake amri na ile sheria
Ni kutuzoeza na utamaduni wa mbinguni

Shairi la 3
Dalili moja kwamba kweli unampenda bwana
Utawafundisha watu kuzitii amri zake
Hata bwana mwenyewe
kwa kinywa chake asema,
Kama kweli wanipenda mtazitii amri zangu
Hivyo yatupasa wote tulokombolewa
Kujizoeza nayo desturi ya nyumban
Kumbe safari itafikia Mwisho wake
Anayo heri atakaefika salama
Wewe uhubirie neno ni kama Dereva
Tena wale wafuasi wako ni abiria
Wapaswa kuzithamini sheria za huku njian
Ili ufike salama na abiria wakoo

Kiitikio

Hivyo Ndivyo ilivyo sheria ya Mungu
Ipo kwa usalama wetuu
Mungu mwenyewe haimsaidii kwa lolote
Ila ni kwa faiida yetu,
Lakini siku hizi za Mwisho yapo Mafundisho
Yakwamba amri zake Mungu hazifai tena
Usidanganyike ndugu msafiri Mwenzangu
Bila amri ya Mungu hatutafika salama*2

No comments

Powered by Blogger.