UTABIRI ULITIMIA
kijiweni kwetu
AFE MMASAI NG'OMBE LAKIN AFIKE MNADANI
Kama huna uhakika wa kuangalia mchezo wa leo kwa kwel pole utamisi kitu muhim sana katika maisha yako.... Leo unafiki nauweka pemben... Najua wana Pirlo, sisi tuna iniesta, wao wana Vidal sisi tuna ratikic, wao wana marchisio sisi tuna biskuti, wao wana tevez masikin sisi tuna Messi, wakiweka morata naweka suarez, sisi tumebakiwa na neymar wao wana lorente! Kwa mahesabu ya one againist one tumewazid, sijui tutegemee kipi zaid ya miujiza!
HAKUNA KISINGIZIO
Mpira una njia zake! Kuna kitu kinaitwa form, wote wapo form, wamebeba ubingwa wa ligi, sisi tuna la liga, chini ya massimilano allegri na Luis henriquez...
Juventus ilipocheza na timu za hispania imeshinda mara 15 na kufungwa mara 18 na kutoka sare mara 11, kwenye matuta imeshinda 3 na kufungwa 3. Barca wanarudi baada ya kukaa njee ya fainal mara 4. Messi amezifunga timu za italy magoli 7, timu za hispania zimeshinda mara 22 dhidi ya italy na kudroo mara 13 na kungwa mara 8.
RECORD MUHIMU
Kwa kipind cha miaka ya nyuma wote hawa wamepoteza fainal 5, juventus akishinda mwaka 1977,90,93 na kupoteza 95, na 84 walishinda kombe la uropa. Walipokutana hawa jamaa mwaka 2003 mechi ya kwanza kule turin, walitoka 1-1 nou campe 2-1, goli la Zalayeta na xavi akasawazisha nedved pavel akafunga kazi. Waliokuwepo kipindi kile ni xavi na buffon tu, leo wamekutana tena, istoshe luis henrique nae ALIKUWA ndani...1985 walitoka 1-1 kule hispania, kule turin goli la michael Platin lilifunga mahesabu. Mwaka 91 barca waliua mtu 3-1 mechi ya pili wakalala moja bila
UZOEFU DAWA
Juventus wana wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa Fainal za uefa kama Andrea Prilo akiwa na milan 2003, 2007, evra akiwa na monaco, man utd, tevez akiwa na united, morata akiwa na madrid 2014. Morata anaingia kwenye redord za akina Rivaldo, kwa kuingia kwenye fainali mbili mfululizo na klabu mbili tofauti wengine ni kama Paulo sousa akiwa na juventus 96, akaenda dotmund 97, marcel Desaily akiwa na marseille 93 na 94, mwingine ni samuel eto'o akiwa na Barca baadae inter 2009 na 10. Barca kwa upande wao wana wachezaji 8 ambao wote wamecheza fainal mbili za nyuma wengine mpaka tatuu, daniel alves, pique, xavi iniesta,mascherano,pedro, mess, biskuti na adriano huy benchi lilikuwa lake tu.
MBUZI ATAKULA MKEKA LEO
Kwa kiasi fulani uzoefu wa akina evra, morata na pirlo na mzee tevez unaweza kuwapa ari pogba, vidal na marchisio, lakin najiuliza kwa mtu kama neymar, suarez na arkitic ambao hawajui uefa ni nini chini ya usimamiz mkuu wa Messi na iniesta watakubali kula majan kwel?? Messi anatafuta kufunga fainal ya tatu baada ya kufuwafunga man utd mara mbili. Luis henrique anaingia huku akikumbuka ubingwa alioutwa akiwa kama mchezaj mwaka 1997 dhid ya PsG... INATOSHAAA.... Tembelea
privaldinho.blogspot.com
Leave a Comment