MORGAN SCHNEIDERLIN NI KILAZA TU

Kijiwe chetu
MORGAN SCHNEIRDELIN NI KILAZA

Na Priva Abiud


Jana nilikuwa najadiliana na mshkaji wangu Bwana Lally kuhusiana na nini maana ya world class player na avarage player! Tulishindwana sana, hasa pale nilipomkatalia kuwa Morgan Schneirdelin sio World Class Player ni avarage! Alikuja na fact kwamba kwa takriban misimu mitatu iliyopita

Jamaa aliweza kufanya tackling 274 zaidi ya mchezaji yoyote yule pale EPL! Kwa msimu uliopita aliweza kufanya tackling 79 kwenye michezo 26 hii ni sawa na tackle 3.7 kwa kila mechi huku aliyekuwa akimfata kwa karibu ni matic aliyecheza tackle 3.6 kwa michezo 36. Fransis Coqelin alifanya tackle 3.3 kwenye michezo 22, fernandinho alifanya 2.8 kwenye michezo 33.
************************
Unaposema
Image result for morgan schneiderlinsuala la best defensive Midfielder in EPL, kwanza unazungumzia watu kama Carrick, Tiote, Morgan, Coqelin, arteta, fernandinho, matic, na wengineo. Lakin sio kila best player sehem fulan basi anakuwa World Class. Zipo sababu zinampelekea mchezaji kuwa world class, kwanza ni timu aliyoko, huwezi kuwa world class kama upo ligi ya cyprus huko, au upo maccabi haifa! Kwa mfano mtu aliyepo watford hawez kuwekwa kundi moja na mtu aliyeko madrid, kwanza aina ya michezo watakayo cheza, huyu atakuwa anacheza na tension kubwa ya mashabiki, media, kukamiwa uwanjan, na big games, wa watford yeye hawazi, wapige barida, cha msingi ulaji.
***************************************
Image result for morgan schneiderlin Kingine
kuna kitu kinaitwa best upcoming players! Morgan yupo hili kundi. Ni wasaa wake sasa kujenga jina! Memphis depay kashajenga jina, now anatengeneza utawala wake! Msimu uliopita alikuwa mfungaji bora kwenye Ligi ya Uholanzi. Nilisikia Man utd wanamtaka Mane wa southampton, nilibutwaa! Maana kilichomtokea liverpool ni kujaza best upcoming player ambao impact zao sio kubwa uwanjan, kwanza haogopwi, pili hawana experience na game kubwa tatu wanacheza kujenga majina na sio kuleta mafanikio kwenye timu!
****************************************



Image result for morgan schneiderlin Leo hii united wamejaza akina darmian, shaw, morgan, depay, herrera, januzaj, blind, Rojo, wote hawa ni wachezaj wanaotaka kutengeneza majin, hawa wote ni best upcoming, wamefanya vizuri hivi karibu, wengine hata hawakujulikana mpaka pale walipokuja. Nikuchekeshe tu, wakati depay anakuja Man u, kwenye acckount yake ya instagram alikuwa na Followers lakin 3 alizidiwa hata na diamond, lakin sasa hivi anafollowers takriban million 1 na uchafu.. Kwa mahesabu hawa wanatosha kabisa, maana watacheza na experienced players kama Rooney, mata, bastian, carrick, ila pale nyuma atleast smalling amepata momentum, kilichobaki ni kutafuta beki mkubwa dunian, achana na hawa akina otamend! Vunja ukimya uza DeGea leta Ramos, ukishindwa leta bale! Asante
*************************************

Image result for morgan schneiderlin
Nirudi kwa morgan,
Jamaa anakoelekea atakuwa kiungo bora kabisa dunian kama van gaal atamwamin, kwa mfano tu, anaongoza pass accuracy kwa 89% matic 86% fernanindo 88%, amefanya interceptions 2.6 kwa kila game ukilinganisha na coqelin 3.0, amefanya clearence 47 huku coqelin 68, pasi muhimu amepiga 0.8, fernandinho 0.9, coqelin 0.2. Amemiliki mpira kwa rate ya 3.75 akiwa anaongoza! Kimahesabu hili ni zao zuri tu kutoka kwa mzee Koeman,... KWA HIYO NDUGU ZANGU MUACHE KUSEMA MORGAN NI KILAZA
‪#‎dinho‬

No comments

Powered by Blogger.