SHAW USITAKE KUONEWA HURUMA
San Andy
Wakati nakua (kipindi cha balehe) nilikuwa na msichana fulani hivi tukaenda enda baadae kuna jamaa akaja akamchukua yule msichana ilikuwa inaniuma sana kwasabu jamaa alikuwa ana nitambia,Nikaamua kuanza kutia huruma kwa yule msichana ili arudi kwangu ila mbinu yangu haikufanya kazi hata kidogo
Nikakaa na kujiuliza kama jamaa ni mwanaume kama mimi sasa amenizidi nini hadi kamchukua yule msichana? Nilichogundua ni kuwa jamaa alifanyia kazi udhaifu wangu (Nilikuwa nampenda yule msichana ila sikuwa najali) jamaa akawa ana care sana,Kwakua yule alikosa care kwangu akaenda kule,Kama unavyojua hakuna mkamilifu namimi nikasoma udhaifu wa jamaa na yule msichana akarudi kwangu,Tokea wakati ule nilijifunza kuwa "Udhaifu wako ni nguvu ya mwingine" na "Mwanaume usiombe kuonewa huruma ila pambana" Tuyaache hayo ya Andrew twende kwa San Andy
Kabla ya August 2015 kwenye mechi kati PSV dhidi ya Manchester United ambapo ulimwengu wa sokka ulishuhudia moja kati ya injury mbaya kwenye mchezo huo,Nazungumzia mguu wa Luke Shaw uliovunjika mara mbili akiwa kwenye harakati za kuwania mpira dhidi ya Hector Moreno,Kabla ya tukio lile hakuna mtu aliyekuwa akiuliza beki wa kushoto wa Man Utd ni nani maana jibu lilitoka kwenye miguu ya Shaw alikuwa hatari mnoo
Mambo yameenda kombo kwa Shaw kuanzia siku aliyoumia aliyemvunja alikuwa man of the match gundu likaanza hapo,Shaw amerudi akiwa sawa lakini bahati mbaya sana ameshindwa kuwa na namba ya uhakika kwenye kikosi cha Mashetani wekundu,Matheo Darmian na Daley Blind wamekuwa wakipokezana kucheza kwenye eneo la Shaw
Mtu kama Darmian hana uwezo mkubwa sana wa kucheza beki wa kushoto kumzidi Luke Shaw lakini Darmian anajituma kwa kadri ya uwezo wake,Kuna aina ya wachezaji ambao hawana uwezo mkubwa sana ila akiingia uwanjani anatumia ule ule uwezo alionao mtazame Olivier Giroud ni kama Darmian hana uwezo mkubwa sana ila siku zote ana hakikisha anatumia uwezo wote alionao ingawa sio mkubwa sana,Waswahili tunasema kheri ya hamsini nzima kuliko mia mbovu
Shaw ana speed sana kama akiamua kuitumia anaweza kupata namba tena kwa Mourinho hiki ndicho kitu smbacho yeye anacho wengine hawana kama ataamua kufight ana nafasi maana ana kitu anachozidi wenzie,tatizo ni kuwa Shaw kakaa anategemea mashabiki wamuonee huruma na waanze kumpush Mourinho ampe nafasi,Kwa Mourinho tunaemfahamu unafikiri ana muda wa kumuonea mtu huruma wakati yeye anahitaji mtu anaepiga kazi na kumpa matokeo
Jana Jose Mourinho amesema "ili Shaw arudi kwenye ubora wake anahitaji kucheza mechi sita mfululizo na nikitu ambacho akiwezekani kwakua kwenye nafasi yake wapo wawili" ila tujiulize tu kama Shaw atapata nafasi hata dk 30 na akamua kutumia udhaifu wa wenzake kama strength yake na sio kutia huruma,Mechi ijayo hapati namba? Mfano mzuri ni Athony Martial aliamua kuacha kutia huruma na kufanya kile Rashord hawezi leo hii tunajua hazipiti mechi mbili bila kucheza
Naamini kama Shaw atafanyia kazi udhaifu wa Darnian ns Blind hizo dk 30 atazopata zitatosha kumshawishi kocha ampe dk 45 mechi inayofuata,kama ataendelea kufanya vizuri ataendelea kucheza hadi kufikia kurudisha nafasi yake kwrnye himaya yake
Yote kwa yote bahati mbaya sana kwa Shaw ni kuwa kazaliwa Uingereza sehemu ambayo mashabiki hutaka mchezaji wao acheze bila kujsli uwezo wake na Shaw kaamua kutia huruma mbele yao ili wamsaidie,Nchi kana Brazil ukikosa namba kwenye klabu yako hakuna wa kukuonea huruma pambana mwenyewe,Mwaka jana Neymar wakati snazingua watu walifuta Neymar kwenye jezi kisha wakaandika MARTA
Niliwahi kuambiwa mwanaume wa kweli.ukimpa nafasi ya kuchagua kati ya kum chalange au kumuonea huruma,Atachagua kum challange nafikiri huu ni wakati ambao Luke Shaw anapaswa kuacha kutia huruma ili arudishe kilicho chake
#DarEsSalaamDerbyDay
Leave a Comment