Thursday, 14 September 2017

ACHA KUISHI KWA MAZOEA JIKAZE

*Usipende mafanikio ya ghafla. kubali kufurahia kila sehem ya maisha unayopitia...

*si unamjua Jarmie Vardy? wewe si umezaliwa Kibondo kigoma? na umekuja mjini na treni? basi mwenzio alizaliwa Sheffield Uingereza. alianzia soka pale Stocksbridge inayocheza ligi daraja la 8 mwaka 2007. akiwa na Miaka 20 tu alikuwa mfungaji bora wa timu na alisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa na kuipandisha daraja la 7.

*Baadae alisafiri mpaka klabua ya Halifax Town inayocheza daraja la 7 mwaka 2010 wakati nyie mkisema hari mpya nguvu mpya na kasi. hapo pia alikuwa mfungaji bora na aliwapa kombe na timu hiyo kupanda daraja la 6. akifuga jumla ya magoli 24

* kisha akaenda Fleedtwon iliyokuwa daraja la 5 mwaka mmoja baadae. Alipeleka timu daraja la 4 kwenye Historia ya klabu hiyo akabeba kombe huku akaongoza ligi kwa magoli 31. yupoa pale pale England anahangaika kuja ligi kuu wewe upo kasulu unaambiwa fanya uvuvi kwa bidii hutaki unataka kuja Dar tu baada ya kumaliza la saba. uje ufanikiwe karahisi nan kakwambia Dunia imekuwa rahisi hivyo?

*sio mbaya mwisho alifika mjini Leicester. huenda alifurah kama wewe ulivyofika dar mara ya kwanza baada ya kuuza Mikungu ya ndizi Kule Matola mbeya mjini ili upate Nauli ya Luwinzo uje mjini. hakuwa na maisha mazuri sana Leicester licha ya kufunga magoli 16 yaliyoiwezesha kutwaa ubingwa na kuitoa kutoka daraja la kwanza na kwenda ligi kuu

*Alipofika ligi kuu hali haikuwa nzuri kama kijana wa rombo aliyeuza mbege ili aje afungue duka mjini. 2014 alihakikisha kibanda chake cha Leicester kisishushwe Daraja. 2015 alitwaa Ubingwa ambao ni mgumu kuliko yote duniani...tena akiwa mfungaji bora namba mbili nyuma ya Kane Harry.



No comments:

Post a Comment