Na Privaldinho Abiud
Walio wengi tumezaliwa tukawakuta wazazi wakikesha juani na wengine hata wakiokota makopo ili tu tuweke kitu kinywani. Samahani kama umezaliwa Osterbay. Pia samahani kama hukupata bahati ya kuishi na wazazi. Antonio Valencia siku hizi anaonekana amejichubua usoni. Sawa tu. Si pesa zake bhana? Au kamkopa mtu?
Mara nyingi tumekuwa wepesi kusema Diamond bwege kazingua anajishaua, ana masifa, kiherehere,,, wengine Ali kiba boya tu hana mbele wala nyuma, hana hela, anajisikia. Sawa tuna haki hiyo. Si ndio. Bando si lako bhana? Ndio we ponda tu.
Ila nyuma ya mafanikio ya mtu kuna mnyororo mrefu sana. Huenda Valencia hakuwahi kuwaza kuichezea hata lipuli ya huko kwao sembuse Man utd . Huenda labda na wewe upo Kyela Mbeya na unasuburia Migomba yako kama mitatu miwili ikomae upate ndizi ukauze Matolo kwa bei upate Nauli ya kuja Dar. Oyaa big eeh Usikate tamaa. Kutoka Mbeya hadi Dar hazifiki Km 1000 lakini huenda unawaza sana utafikaje lini na wapi, pole ila usiogope. Lakink pia Nina uhakika licha ya kwamba tuliambiwa tukikaa mjini mpaka october sisi wanaume ila hizi kauli zisikutishe, nakusihi sana wewe mwaki nani sijui, lima mpunga kwa wingi ipo siku utamiliki ghala lako kule tunduma kama sio Magugu Arusha.
kwanini usikate tamaa? Ukizungumzia mji maarufu kwa madawa ya Kulevya kule nchini Ecuador huwezi kuacha kutaja Neuva Loja. Ni mji wenye ubabe na uchafu wa kila namna. Sasa valencia alizaliwa kule. Hakuwahi kufikiria kwamba ipo siku atatembelea kilometa 8,926 mpaka jiji la Manchester. Yaani ni kama wewe uliyepo masasi unawaza kwenda kuchukua watoto wa kali kule Copa Cabana Brazil. Unaweza kuona ni ndoto.
huwa najiuliza sana kati ya Idadi ya watu wa mji wa Sucumbios inayofikia 57,727 Mabosi wa Man utd walimwonaje Valencia? Usikute na mimi Kuna watu kutoka Uholanzi wananifuatilia bila mimi kujua eh? Ndio maana nimekwambia haijalishi hata kama upo Ikwiriri amini ipo siku utakwenda Jijini Mwanza ukamiliki mjengo wako wa maana Kule Capri Point au hata hapo Osterbay tena usali St Peters na Magufuli.
Viatu vya shule alivyonunuliwa Valencia na wazazi wake kwenye soko la kule Quito Pinchincha ndivyo alikuwa akivitumia kuchezea mpira kwenye kiwanja cha Carlos Vernaza ambacho mama yake alikuwa na glosari pembeni
Mama yake alikuwa muuza Pombe za kienyeji sawa na Mama Priva tu aliyewahi kuuza mbege! Nadhani kazi yake Valencia ilikuwa kama sio kubeba ndoo za Pombe basi ni kusambaza oda.
*kumekuwa na Wimbi la vijana wengi wapo mtaani wanaokota makopo na kwenda kuyaauza. Kwa akina Valencia Hili lilikuwa bonge la dili maeneo kule Quito wakati yeye na baba yake walikuwa wakiyatafuta makopo hayo kwa udi na uvumba. Huenda walikuwa wakimzungumka mama kwa kwenda kuyauza makopo hayo wakati mama yao yeye alikuwa akiyahitaji kuuzia mbege yake.
Huenda wewe unayesoma hii umefanikiwa kuliko mimi, ila kubaliana na mimi kwamba riziki ya mbwa ni miguu yake. Mapafu ya Valencia na jitihada zake ndio umaarufu wake kule Equador. Licha ya mafanikio na umaarufu alio nayo kwa sasa sio mtu wa kujivuna. Jamaa muda wote uwanjani amechomekea, hana tatizo na mtu. Ana chenga yake mojaa tu.. ile paap paap kama anaruka fulani hivi. Hiyo hiyo inamfanya aibadilishe familia ya mzee Valencia kule Quito.
Ni mara chache sana kumuona Valencia akifunga goli akionesha ishara yoyote kama swaga au manjonjo. Haamini sana katika kamera. Anafahamu kamera sio maisha yake. Anajua kuwa kamera zinapaswa zimfuate yeye. Akifunga goli hana ishara, hana swaga, yeye anarudi namba nyuma kuja kusubiri mzigo uanze. Anapiga kazi. Rivaldo alifukuzwa Barcelona kwa kugoma kucheza kama namba 11, valencia nina uhakika hata leo akiambiwa adake yeye fresh tu. Yeye ni kazi .
asili yake ya mwanzoni ya kutokuchagua kazi inamfanya leo awe beki wa kulia bora kabisa machon pangu kwa wakati wake. Tunaweza kuwataja akina Dan Alves, Na carvajal kama Mabeki wa kulia wazuri duniani lakini tusipomweka Valencia kwenye kundi hili kwa sasa nasi inabidi tuanze kuokota makopo.
Ni kwambie tu, Valencia alikuja mjini hamjui mtu yoyote yule, tena hata nauli ya gari alilipiwa na Carlos.
*Sio kwamba hapendi umarufu ila anapenda kuishi maisha yake. Alipewa namba saba. Alipoaanza kufananishwa na Ronaldo alikataa ni mwisho aliomba abadilishwe namba 25. Nikimwangalia nahis namwona Paul Scholes ambaye yeye na Umaarufu ni Diamond na Seduce Me. Valencia alimaanisha hivi usilewe sifa kwa kufananishwa na watu waliokuzidi ikiwa hujawafikia.
*huenda kuna kitu kidogo unacho maishani kama Chenga Moja ya Valencia amini huo huo ndio mtaji wako..
No comments:
Post a Comment