hisia zangu na brazuka

katika Uwanja: Maracana Jiji: Rio de Janeiro wenye Uwezo: Watazamaji 73,531
 una historia ya kipekee katika soka la Dunia. Maracana ilijengwa upya kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia mwakani. Ulifunguliwa Juni mwaka huu kwa mechi ya kirafiki kati ya Brazil na England.
Ndiyo uwanja utakaotumika kwa fainali Julai 13 mwakani, mandhari yake nzuri ndicho kitu kinachovutia zaidi kwenye mji huo kutokana na kuwa na fukwe safi na vivutio vingine vya kitalii kama Mlima wa Sugar Loaf na Sanamu ya Christ the Redeemer.
Maracana ulitumiwa kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 1930, ambapo mashabiki 200,000 waliingia na kuishuhudia Uruguay ikiichapa Brazil
kabla kipute hakijaanza najaribu kujiuliza kwa uapnde wa timu 4, brazil, italy, france, england, hizi ni timu ambazo zinachukuliwa katika hali tofauti tofauti, italy mimi shida nao, ufaransa hawana ribery hawana nasri kiukweli nao sina shida nao ukitupilia mbali wana mtu kama cabaye, matuidi ila sio kioo katika michuano mikubwa, ndugu zangu england hapa napata kigugumizi, kiukweli bila unafiki wana defence nzuri sanaa, angalia wana luke shaw, jargielka, johnson, flanagan, cahil na baines, wote hawa ni visiki vikubwa pale england, ukija katikati nahisi kuna kitu wamebugi, hususan kumuacha barry huku wakimtegemea mzembe henderson, sion kama akikaa na lampard au gerrad watafanya la maana, mbele wana sturidge wana ramires wana rooney wana wilshare sion sababu ya kuibeza england
 najiuliza watu kwanini wanakata tamaa hawa jamaa naona wengi wanapiga kelele na ubelgiji kisa wanamajina mengi yalipo EPL, hivi kwan kucheza EPL ndo kuwa bora au kuchukua ubingwa??? sitegemei kuwaona popote hawa ubelgiji,





wanasafari ndefu sana kufikia mafanikio ya kaka zao na baba zao, hapa nawazungumzia masela zangu akina neymar na luiz,
 ukirudi miaka 10 nyuma palikuwa na mtu kama rivaldo na kaka wengine wakubwa, nikilinganisha aina ya wachezaji wa scolari wa sasa na wale aliowachukua miaka ya nyuma wakati anamuacha romario na kumchukua bwana mdogo ronaldinho na akabeba ndoo leo anamsaliti ronaldiho anaondoka na bernad, oscar, neymar na machalii wengine ambao ukichanganya viwango vyao wote hawafiki hata robo ya dinho, sio sababu mimi natupa karata yao kwa mabeki wao, luiz, silva, laves na marchelo, ila najiuliza je akiumia beki mmoja wa pembeni itakuwaje maana benchi watakuwa na mtu kama maicon, na maxwel, sioni sababu ya felipe na miranda kuachwa, sawa katikati ni wazima sana ukiamuangalia fenendinho, na ndugu zake wengine, mimi sina iman nao sana ila kwakuwa ni ardhi ya nyumban naweza kuwaona robo huku wakitoka wakilia na hili litakuwa fundisho kwao kwa miaka ya mbele, sina shaka kwa coutinho, na moura kuachwa maana sio kitu mbele ya oscar, na bernad, zime baki siku chache sana england tayari wameshaenda copa cabana, sasa hivi watakuwa wanajua kusema nabarte na mashorte, kikwazo kikubwa kwa wabrazili ni maandamano yanayoendelea, anahaki ya kuandamana kwakeli maana hii ni mojawapo ya nchi zenye uchumi mbovu,angalia ndugu zetu africa kusini mpaka leo wanamadeni makubwa juu ya maandalizi ya kombe lililofanyika pale, natamani sana priva mimi ningepata nafasi kuangalia angalau mechi moja ya spain na brazil pale pale copa cabana kwa macho yangu haya haya sio kwenye tv wala cinema maana kitendo cha sopain kufungwa tatu basi dira ya nani bingwa imegeuka, ndugu zanguni ujeruman polen sana kwa kuwapoteza gundogan na reus, nmesikia ronaldo atalindwa na mabaunsa kule rio de jeneiro sasa sijajua sababu kubwa n wanawake wa kule au umaarufu, nikasikia tena wafaransa wao hawataki sabuni za vipande wala unga wanataka sabuni za maji, walgeria nao hawakuwa nyuma wanataka kuran kila chumba, wengine wakasema hapana tuantaka tuletewe ndizi zetu kutoka equador hatutaki ndizi mshare za kichaga wala kisukuri za bukoba, waustralia wakasema ttunataka kahawa tu.
hivi unakumbuaka<<Ilikuwa ni mechi kati ya Ufaransa na Italia ambapo watu tulishangaa bwana Zinadine Zidane akimnyuka mchezaji wa timu ya Italia kichwa cha kifua na kupelekea kupewa kadi nyekundu.Watu tulibaki kushangaa kwanini kafanya vile kutokana na heshima aliyokuwa nayo kisoka lakini baadae ilikuja gundulika yule mchezaji wa Italia alimwagia matusi bwana Zizzou tendo lililomkasirisha na kumpelekea kumuadhibu na kichwa cha kifua.

Ricardo Kaka mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil alikula kadi nyekundu kwa kitendo ambacho kilikuwa cha kijinga tu maana alimpiga kipepsi mchezaji wa Cote d' vore ambae nae niliona kama kaigiza kwa kule kugaragara kwa maumivu,ndio alipigwa kipepsi lakini hakikuonyesha kama kilikuwa na aina ya maumivu aliyoonyesha kusikia.Kaka jana ilikuwa siku mbaya kwake kabla ya kula kadi nyekundu tayari alikuwa ashapewa kadi ya njano kwa vurugu zake nahisi jana aliamka vibaya. huu ni mtazamo wangu tu
by Priva Abiud @udom

No comments

Powered by Blogger.