magoli ya ajabu copa cabana
Natumaini kila mmoja anajua kinachoendelea kule kwa watoto wazuri copa cabana, wakati kombe linaanza kwa ufunguzi huku wenyeji wakipamba kombe lao kwa uoto wa asili wa misitu mbalimbali kama amazoni, neymar alipamba ufunguzi kwa goal zuri sana likiwa ni goli la kusawazisha,hongera kwake neymar hakuishia hapo, alifunga bao la penati ingawa haikuwa penati nzuri sana lakini ilikuwa nzuri kwa watazamaji wa soka waliokuwa wakiishabika brazil, oscar akaamua kufunga ukurasa kwa bao zuri kabisa la mechi, ni kazi ya ramires aliyemkabia oscar akaondoka na mpira akafanya choping ndogo tu, sherehe hiyo ya magoli mazuri haikuishia hapo, mshambukliaji wa kimataifa wa uholanzi robin van parsie aliweza kufunga goli ambalo limekuwa gumzo kabisa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, wapo waliomuita van air, alikiruka kama ruler 3 kutoka usawa wa ardhi akaenda hewan kama ndege akapiga free header casilas akapishana na gari mshahara
hivi ndivyo van parsie alipopeleka kilio katika miji ya madrid na barcelona, sio goli rahisi kwa mchezaji wa kawaida, alifanya kitu ambacho van gal atazidi kuvutiwa na kijana huyu hasa pale katika kiwanja cha old traford atakapoenda kama kocha mkuu wa man united msimu huu,hii ilikuwa siku mbaya sana kwa mabingwa watetezi ambao walitoka uwanjani kwa goli la penati la xabi alonso wenzao wakitoka na magoli matano,
bila kusahau magoli ya roben ambaye yeye ndie alikuwa muamuzi wa casilas alale, atambae au akae,

hizo nizo adhabu alizopewa babu casilas aliyekuwa team captain, hali ni ngumu sana kwa vijana wa del bosque, hali n tete disco limeingia mmasai, tunakumbuka vizuri sana kuwa fainali zilizopita roben ndiye alienyima uholanzi ubingwa akikosa nafasi za uwazi mbele ya casilas leo hii anaamua kumdhalilisha kabisa kwa kumpeleka atakavyo, sjauona mwisho wa spain bado nasubiri kujua wataishia wapi, je yaliyomkuta bingwa italy kule afrika kusini yatamkuta na casilas hapa brazil???
goli lingine zuri kabisa n goli la marchiso dhidi ya uingereza, padri pirlo anafanya mpira kuwa mchezo mrahis sana dunian kwamba hata vikongwe wanaweza kufanya wanavyotaka, ilipigwa pasi yaa v alichofanya babu pirlo alisusa kilichomkuta joe hart mimi sijui ni goli la aina yake limepigwa mbali sana
huyu babu utadhani ana miaka 18 hivi hasa pale napokumbuka aliponiacha hoi kwa penati aliyomfunga joe hart katika michuano ya euro, huyu ndiye naepaswa kulipa dola laki 3 kwa wiki sio akina rooney, asante sana babu nmeona kazi yako, R campbel nae alifunga goli zuri pia dhidi ya uruguway, weka pembeni goli la costa rica dhidi ya greece ambalo zilipigwa wonderful passes,
Jana usiku mcheaji bora mara nne ambaye amekuwa akishutumiwa na mashabiki wengi kuwa hana msaada kwa timu yake ya taifa nae anaingia kwenye list hii chache ya magoli mazuri walipokuwa wakicheza na bosnia,
lillikuwa shuti zuri sana, kama tunavyojua messi huwa ni mchezaji anae amua afungeje, shuti, achopu, au achukue kijiji, maisha ni mtandao kwa sasa mambo yanaenda kidigital zaidi, kila kitu kimebaki kuwa historia, habari ya kukariri maisha haipo, messi amenadamwa na tatizo la kutapika uwanjani huku adui yake mkubwa christiano ronaldo yeye akilindwa na polisi wa rio de jeneiro, usalama wa taifa wa brazil, na maafisa wengine wa usalama kutokana na timu yake ya taifa kukaa katika kambi yenye matukioa ya kiuhalifu.
by Priva Abiud@udom
hivi ndivyo van parsie alipopeleka kilio katika miji ya madrid na barcelona, sio goli rahisi kwa mchezaji wa kawaida, alifanya kitu ambacho van gal atazidi kuvutiwa na kijana huyu hasa pale katika kiwanja cha old traford atakapoenda kama kocha mkuu wa man united msimu huu,hii ilikuwa siku mbaya sana kwa mabingwa watetezi ambao walitoka uwanjani kwa goli la penati la xabi alonso wenzao wakitoka na magoli matano,
bila kusahau magoli ya roben ambaye yeye ndie alikuwa muamuzi wa casilas alale, atambae au akae,

hizo nizo adhabu alizopewa babu casilas aliyekuwa team captain, hali ni ngumu sana kwa vijana wa del bosque, hali n tete disco limeingia mmasai, tunakumbuka vizuri sana kuwa fainali zilizopita roben ndiye alienyima uholanzi ubingwa akikosa nafasi za uwazi mbele ya casilas leo hii anaamua kumdhalilisha kabisa kwa kumpeleka atakavyo, sjauona mwisho wa spain bado nasubiri kujua wataishia wapi, je yaliyomkuta bingwa italy kule afrika kusini yatamkuta na casilas hapa brazil???

huyu babu utadhani ana miaka 18 hivi hasa pale napokumbuka aliponiacha hoi kwa penati aliyomfunga joe hart katika michuano ya euro, huyu ndiye naepaswa kulipa dola laki 3 kwa wiki sio akina rooney, asante sana babu nmeona kazi yako, R campbel nae alifunga goli zuri pia dhidi ya uruguway, weka pembeni goli la costa rica dhidi ya greece ambalo zilipigwa wonderful passes,
Jana usiku mcheaji bora mara nne ambaye amekuwa akishutumiwa na mashabiki wengi kuwa hana msaada kwa timu yake ya taifa nae anaingia kwenye list hii chache ya magoli mazuri walipokuwa wakicheza na bosnia,
lillikuwa shuti zuri sana, kama tunavyojua messi huwa ni mchezaji anae amua afungeje, shuti, achopu, au achukue kijiji, maisha ni mtandao kwa sasa mambo yanaenda kidigital zaidi, kila kitu kimebaki kuwa historia, habari ya kukariri maisha haipo, messi amenadamwa na tatizo la kutapika uwanjani huku adui yake mkubwa christiano ronaldo yeye akilindwa na polisi wa rio de jeneiro, usalama wa taifa wa brazil, na maafisa wengine wa usalama kutokana na timu yake ya taifa kukaa katika kambi yenye matukioa ya kiuhalifu.
by Priva Abiud@udom
Leave a Comment