HALI YA CHRISTOPHER ALEX YAZID KUWA MBAYA
WACHEZAJI wa zamani wa Simba
wameandaa mchezo wa kirafiki wenye lengo
la kumchangia mchezaji mwenzao,
Christopher Alex anayesumbuliwa na
maradhi ya kifua kikuu.
Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam Januari 14,
mwaka huu, dhidi ya veterani wa Yanga na
kiingilio kitakuwa Sh 2,000.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mchezaji
wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa
amewaomba mashabiki wa soka kujitokeza
kwa wingi ili kumchangingia mchezaji huyo
ambayo ni miongoni wachezaji walioifunga
Zamalek mwaka 2003.
“Ninawaomba mashabiki waje kwa wingi ili
kumchangia mchezaji mwenzetu apate fedha
ya matibabu na kujikimu kuliko kujitokeza
kumchangia wakati akiwa amekufa, kwani
kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeonyesha
kuwa michezo kweli ni undugu,” alisema
Pawasa.
Naye Juma Kaseja ambaye akiwa miongoni
mwa wachezaji waliokuwepo kwenye kikosi
hicho maarufu kama Simba ya Zamalek,
amewaomba wote waungane kumchangia
mwenzao kwani, maradhi au matatizo
yameumbwa kwa ajili ya wanadamu hivyo
kusitiriana ni muhimu.
Christopher Alex anasumbuliwa na maradhi
ya kifua kikuu ambayo yanasababisha afya
yake kudhoofika, hivi sasa yupo nyumbani chanzo ni habari leo
Leave a Comment