MESSI KUJIUNGA NA CHELSEA
TETESI ZA SOKA ULAYA - KATIKA DIRISHA DOGO
LA USAJILI
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 27,
amezusha tetesi kuwa anataka kuhamia Chelsea
(The Sun), Javier Hernandez- Chicharito, 26,
atauzwa na Manchester United mwishoni mwa
msimu wakati mkataba wake wa mkopo
utakapomalizika Real Madrid (Daily Telegraph),
Tottenham na Liverpool wapo tayari kupambana
kumwania mshambuliaji wa West Brom, Saido
Berahino, 21, (Independent), Inter Milan imewapiku
Liverpool kumsajili winga wa Bayern Munich
Xerdan Shaqiri, 23, (Talksport), meneja wa
Juventus Massimiliano Allegri amethibitisha kuwa
klabu yake inataka kumsajili kiungo wa
Galatasaray Wesley Sneijder, 30 (Guardian), Kipa
wa Arsenal Woijciech Szczesny amepigwa faini ya
pauni elfu ishiriki kwa kuvuta sigara akiwa bafuni
baada ya mechi dhidi ya Southampton, siku ya
mwaka mpya walipofungwa 2-0 (Daily Mirror),
Tottenham watawajaribu Aston Villa kwa dau la
pauni milioni 3 kumtaka kiungo Fabian Delph, 25
(Daily Mirror), Chelsea wamewazidi kete Arsenal
na Liverpool katika mbio za kumsajili kiungo wa
Saint-Etienne Rayan Souici,16, ambaye
amepachikwa jia la "Paul Pogba mpya" (Daily
Express), Wilfried Bony amewaambia Swansea
kuwa anataka kuhamia timu inayocheza
Champions League (Daily Telegraph). Tetesi
nyingine kesho nikijaaliwa.
Leave a Comment