NAJIULIZA WATAKUMBUKWAJE

Kijiwe chetu

NAJIULIZA WATAKUMBUKWAJE?

Wakati dunia ya sasa kisoka ikikaribia kumpa Ronaldo tuzo yake, dunia ijayo ina fumbo gumu sana kwamba tutampa nan? Wapo wanaosema kuwa Messi atarudi, wapo wanaosema neymar, wako pia wanaothubutu kusema Hazard! Ila  mimi niwe muitaliano niseme Bellum Se Ipsum alet.... Yaan kingereza tunasema War will feed on itself... Kibongobongo tunasema liwalo na liwe, kihuni zaid tunasema chapa ilale!!

WAASISI WA SOKA
Ukweli utabaki kuwa dunia nzima inamjua Pele ni nan! Hata mngoni wa mbamba bay kwa akina ngonyan anamjua maradona ni nan! Wakati mimi nazaliwa nilikuta majina kama ronaldo de lima, akina Garrincha, Zicco, na wengineo Wenye sifa kubwa wakitajwa na kukumbukwa! Ila cha ajabu niliyemsikia kutoka afrika ni Okocha Peke yake! Wengine wote nimetumia jitihada binafsi kuwajua!

TATIZO NI NINI
Kubali ukatae africa ina historia kubwa ya kisoka tatizo linakuja kwenye uinuaji, utangazaji, na Pesa! Kwa mfano ukijaribu kuangalia, juzi juzi nilibahatika kusoma kitabu cha AFRICA SOCCER HISTORY cha proffesor Peter Alegi anasema mpira umeingia afrika miaka ya 1862, na mechi ya kwanza kubwa zilichezwa afrika kusin mwaka huo.utagundua soka limeanza muda ila ukuaj wake umekua finyu mno.. Kuna kitu kinanisumbua sana, miaka nenda rudi mbali na bara la afrika kuwa na vipaji lakin vipaji vile vimeishia kuuza karanga!

Inasikitisha kwa kwel
Juzi juzi rafiki yangu mmoja alinambia kuwa alikuwa na ndoto za kucheza soka la kitaifa (simba na yanga) ila anasema wakati akiishi dodoma alikutana na christopher alex (simba ya zamalek)! Akaniambia kuanzia siku ile alienda kuuza viatu vyake vya mpira na jezi akaenda kukatia nazo n g'ombe mgomba kule meru kutokana na hali aliyomuona nayo alex inasikitisha mno mchezaji mwenye jina kubwa lakin maisha magumu!

MIKAKATI MIBOVU
Wachezaji wengi wamefanya makubwa lakin hatuwakumbuki, kuna mtu anaitwa Roger Miller ila siamin kama vijana wa sasa wanamjua, ila wanamjua romario, wanamjua bobby robinson, akina george best, nina uhakika kuna watu hawafaham kama George Wear alishawah kuwa
mchezaji bora wa Dunia! Hatuwakumbuki kwa sababu tumeng'ang'ania EPL, LA LIGA N.K.. Na tunaamin kila anachosema na kutangaza mtu mweupe basi ndicho Sahihi.. Hakuna project za kuwatangaza waasisi wetu,kinachobaki wanarudi kijijin kwao kunywa mbege! Tunawajua zaidi waasis wa wenzetu ila wetu hatutaki hata kuwajua! Old is Gold siku zote! Wale wana nafasi kukubwa kukuza soka kwa vijana wadogo kwa kuwapa motisha na hamasa kama ilivyokuwa kwa Pele, rivaldo dunga, kwa akina neymar osca n.k au Abed pele kwa wanawe Wale!

MALEGEND WA AFRIKA!
Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika ilianzishwa mwaka 1992 mwanzon ilikuwepo tuzo ya Golden Ball ilyokuwa ikitolewa na gazeti moja la ufaransa kuanzia mwaka 1970 mpaka 1994. Wapo watu wakukumbukwa Sana kama Weah, Abedi Pele! Kuna watu kama Nwankwo kanu, achana na mkorofi Diof, akina Taribo West aliyewapa wazungu matango akawadanganya ana miaka 28 wakati mama yake alimzaa miaka 42 iliyopita, unamjua thomas N'kono alyeshinda ile tuzo mara mbili?? Angalizo,,,Hana undugu na Nimbrod N'kono, kulikuwepo na Mpambanaji Patric Mboma! Achana ronaldinho wa Afrika JJ okocha, akina papa camara wa gunea, mkongo mwamba kazadi wapo wengi Sana tatizo je tunawajua???

MASWALI YA KUJIULIZA
Mwaka huu Yahya Toure kamfikia Samueli Eto'o akiwa na miaka 31... Naamin tena mwakan atabeba tena maana simuon mpinzan wake maana kamshinda aubemeyang na Enyeama wote ni hawawez kumpiku! Ila najiuliza Kwa namna yahya toure alivyofanya, Amefanya makubwa kidunia ingawa hana kombe la dunia je atakumbukwa?? Je ipo siku miaka 60 ijayo waseme alikuwepo toure kama ilvyo kwa Pele?, haya, wamepita drogba na mpinzan wake eto'o, je watakuja akina nan? Je hawa wakiondoka watakumbukwa au watakua kama akina sunday oliesh, amokachi,rashid yekin na wengineo?? Leo hii George Weah hana Jina kubwa dunian, Je yahya toure nae watamsahau kweli?? Wachezaji weusi wanajinamiz la matangazo! Mpka leo Pele anapokea tuzo ballon D' or ila ukiniuliza Mussa hassan M gosi, athuman machupa, Passawa wako wapi ntakwambia wanauza mitumba ilala na kiborolon!,, nani atakaye watangaza waasisi wa soka letu afrika??

Tusitegemee wazungu kabisa,,,ila naomba Mungu Anipe Pumzi nijionee namna akina Yahya toure na eto'o wataondoka na sifa zao mbali na kulipwa ghali.. 

Please follow us on privaletto.blogspot.com for more sports news

Privaldinho @udom

No comments

Powered by Blogger.