RISALA KWA WANALIVERPOOL

Kijiwen kwetu

WAACHE WAHADITHIANE MAANA MAREHEMU KAZIKWA NA VYEO VYAKE

Kuna wakati inabidi ukweli usemwe! Waitaliano wanakwambia "aut vincere aut mori" maana yake kupona au kufa! Kuna msemo mmoja wa ndugu zangu waliofeli wanapenda kuutumia kwamba mavi ya zaman hayanuki ila mm naamin yananuka ukitaka kuamin yamwagie maji utaona! Au wengine wanasema hata bibi alikuwa sister du! Lakin jiulize je sister du wa mwaka 1960 ni sawa na wa 2014??

NYUMA YETU MBELE YAO
Walazwe pema pepon mashabiki wa liverpool 96 waliofariki hillsborough kwenye mechi ya FA April 15 1989 dhidi ya nottingham Forest! Mashabiki 94 walifarik pale pale mmoja alifia hospitalin na mwingine alifariki baada ya miaka 4 baada ya madaktari kushindwa

VIJOGOO
Leo namzungumzia sister du aliyezaliwa miaka 122 iliyopota! Huyu sister du aliolewa na bwana John Houlding baada ya kuachana na mumewe wa zaman Everton! Hapa nawazungumzia the reds au wazee wa merseyside!

MAFANIKIO
Unapozunugmiza mafanikio makubwa ya liverpool unaznungumzia kunako miaka ya 1970-1980 walipokuwa na Bill shankly na Bob Paisley ambao wengi hawawajui, hawa watu waliobeba makombe 7 ya ulaya, na makombe 11 ya ligi! Wana makombe 7 ya FA, 18 LIGI, MAKOMBE MADOGO YA LIGI 8, NA UEFA 5, UEFA SUPER CUP 3 NA UEFA UEFA CUP 3 achana na akina benitez. Mbali na yote hayo ila tokea mwaka 1992 nilipozaliwa mimi mashabiki wa liverpool wakiongoza na Steven Gerrad ambaye alikiri hana jezi ya Man utd kwenye kabati lake basi hawajawah kuchukua Barclays!

MAREHEMU AZIKWA NA GWANDA LAKE!
Kwa kweli kuna watu wanasikitisha sana, hasa majiran zangu arsenal ambao juz juz basi waliondoa mkosi wa takriban miaka 10, ila kuna ndugu zangu hawa ambao wanasifa kubwa sana dunia nzima ambao kwa sasa hata uefa ambayo walikuwa na uzoefu nayo basi wametoka makundi! Mafanikio yao makubwa ya mwisho ni msimu wa 2007 na 2008 walipofika fainal ya UEFA wakafungwa na Milan, na kufikisha point 86 nyuma ya man utd kwenye ligi!

MASHABIKI WAKE SASAA
Ukiwakuta mashabiki waliverpool utakuta wanahadithiana tu, "unakumbuka 2005 tuliwapga ac milan tukiwa goli 3 nyuma na gerrad mgonjwa, sisi ndo tuna uefa nying, sisi ndio tunamfuata man utd kwa ubingwa pale EPL" utasikia tulimfungaga Man utd 4, pale old trafford" yamekuwa yale yale ya gaddaf, mtu kafa na vyeo vyake! Wakati tom hicks na george gillet wanaichukua liverpool ilikuwa na deni la £218.9! Wakaja makocha kama Roy, na Dalgish kuokoa afya ya marehemu lakin imeshindika!

LIVERPOOL YETU YA SASA
Yupo dereva wa boda boda anaendesha sem trela (rodger brendan) tena cha ajabu huyu dereva wa boda boda baada ya tairi ya mbele kupata pancha (suarez) akanunua tairi ya boda boda (lambert) kuiweka pale! "Juzi wakati naangalia game ya liverpool na arsenal nilimwambia rafiki yangu mmoja kuwa mchezaj mwenye hadhi ya kucheza liverpool ni coutinho pekee yake tu!

KWA TAARIFA YAKO
Liverpool ndio klabu ya kwanza England kuanza kuweka logo ya kampuni inayoifadhili kwenye tisheti zao kwa mara ya kwanza! Walivaa HITACHI kunako mwaka 1979

MkASA MWINGINE
Mwaka 1985 mashabiki wa liverpool walianzisha tena vurugu kwenye fainal ya uefa dhidi ya Juventus na wakavunja ukuta na watu 36 kupoteza maisha kwenye uwanja wa heysel liverpool wakafungwa goli moja! Kwa kitendo kile timu za Uingereza zilifungiwa kushiriki michuano yoyote ya ulaya miaka 5!

RISALA
Leo hii liverpool imebakiwa kuongelea historia tu! Sioni kama watarudi leo au kesho! Wapo epl kumfunga Utd kama reeding ilivyofanya kabla ya kushuka daraja! Juzi rafiki yangu mmoja mwanaliverpool aliniambia liverpool tunarecord nzuri sana, 2006 tulitoka 3 3 na west ham, FA na tukashinda kwa penati,2004 tulitoka ac milan 3 3, tukashinda kwa penati, zote hizi ni sifa za marehemu, mwambieni kumwembe kwamba historia ya liverpool imekuwa Risala ajue kwamba "aut vincere aut mori" kufa au kupona"

Wao wanasema You'll never walk alone ila mimi nawaambia you'll stand with your own feet!

No comments

Powered by Blogger.