VITUKO NA MATUKIO KATIKA SOKA
kijiwe chetu
DUM VIVIMUS, VIVIMUS...ILA NDO ILIVYO
Namshukuru Mungu ametuweka tena na tumeona tena mwaka! Waitaliano wao wanasema felices new au felix sit annus novus kule kwa bibi wanasema heri ya mwaka ushiya! Leo napenda tukumbushane matukio madogo madogo na ya kuchekesha sana kwenye soka
Kwanza nianze na hili!
Carlos caszely ndiye mchezaj wa kwanza kupewe kadi nyekundu kwenye michuano ya kombe la dunia kunako june 1974,ni mchezaji kutoka chile!
Kwa taarifa yako..
ASEC Abijan ya ivory coast ilicheza mechi 108 bila kufungwa tokea mwaka 1989-1994... Noma sanaa hii
Kwingineko
Kadi nyekundu 20 zilitolewa kwenye mechi kati ya sportivo ameliano na general cabalero za paraguay..... Kituko cha aina yake kwa kweli...
Inaonesha kwamba timu za ulaya zimefika hatua ya final kombe la dunia kila mwaka ispokuwa mwaka 1930 na 1950.. Ni rekod nzuri na ya aina yake kwa timu za ulaya! Makofi kwao!
Mtu mweusi
Golikipa arthur wharton ndiye mchezaji wa kwanza mweusi kucheza mpira wa kulipwa! Ni mtu kutoka ghana wakati huo ikiitwa Gold Coast, na alisajiliwa mwaka 1889 klabu ya England rotherham united!... Heshima kwake!
Hebu cheka kidogo
Mwaka 1950 india ilijitoa michuano ya kombe la dunia baada ya kunyimwa kucheza peku kama wenzangu kutokea mbeya!......
Maajabu
Mwaka 1957 zikiwa zimebaki dakika 30 tu, charlton athletic wakiwa nyuma goli 5 1, iliweza kurudisha magoli hayo na kushinda kwa jumla ya goli 7 6 dhidi ya huddersfield town...
Umasikin bwanaaaa...
George Wear wa liberia ilibidi awanunulie wachezaj wenzake jezi vifaa vya mazoezi ili waweze kucheza michuano ya kombe la Africa mwaka 1996 wakati huo nikiwa vidudu (chekechea)... Asante wear..
Kiherehere
Celestine babayaro wa nigeria alivunjika mguu alipokuwa akishangilia goli baada ya kuifungia klabu yake ya chelsea katika michuano ya pre-season mwaka 1997! Na akomee!
Kichapo
Refa mwingereza martin sylivester aliweza kujipa kadi nyekundu mwaka 1998 baada ya kumpa kisago cha haja mchezaj na kumtoa manundu hvyo kutokana na sababu za kinidhamu aliweza kutoka nje. kwenye mechi ya Andover Na District Sunday league
Wenge!
Guizeppe Meazza alianguka wakati akienda kupiga penati kwenye mechi ya nusu fainal ya kombe la dunia mwaka 1938... Huo ndo mpira sasa.. Muitaliano huyu alimbwela,,,
Huyu nae hamnazo!
Refa Jean Langenus nae alifanya kituko cha aina yake baada kuvaa koti la suti, golfing pants, na tie yenye michiriz nyekund, alipokuwa akichezesha mechi ya fainal mwaka 1930 kombe la dunia!
Sio ronaldo tu,
Luigi Riva alimvunja spectator mkono kwa shuti lake kali kama la said maulid smg au la pawassa vile!
Ningepiga wote risasi..
Klabu kutoka madagascar inayojulikana kama stade Olympique l'emryne ilijifunga magoli 149 kwenye michuano ya AS Adema mwaka 2002!!
Huyu nae na gundu lake!
Unamjua Michael Laudrap?? Aliichezea Real madrid wakati inamfunga Barca 5 0, pia aliweza kuichezea Barca wakati inaipiga madrid 5 0,,, huyu ni wa kufungia kuzichezea timu zote mbili!
Arsenal mpooooo???
Dennis Bergkamp hakuwahi kupanda ndege alipoichezea arsenal... Sijui ni ushamba ama lah anajua mwenyewe
Fergie naye yumo???
Fergie alifukuzwa st. Marrien 1978 baada ya kukutwa akitongoza demu... Sijui bosi alikuwa akimfuatilia huyo mrembo???? Mimi sijui ila habari ndio hyo!
Heshima kwake!
Stanley metthew hajawah kupewa kadi kwa miaka 33 aliyocheza! Mimi priva Ningekuwa mchezaj mkubwa ulaya ningekuwa kama flamin ahah
Hahahaha
Baada ya arsenal kushindwa kuongoza ligi basi bwana Herbet chapman aliona arsenal wabadilishe jina waitwe arsenal ili angalau wakati ligi inaanza ile table ya mwanzo kabisa wawe juu kwasababu ya herufi A!!! Kama ilivyo chelsea na man cty kwa sasa!!! Huu utani umepitiliza aisee,,
Arsena noma sana
Mechi ya kwanza ulaya kuoneshwa kwenye tv ilifanyika highbury mwaka 1937... Arsenal wapo juu sana..
Marekani ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wachezaji wa kulipwa million 18, kombe la dunia, el classico, manchester darby, manchester united vs liverpool, manchester. United vrsenal ndizo mechi zinazotazamwa na zaid ya watu billion moja dunian.... Asante sana kwa kusoma endelea kutupa support!!! DUM VIVIMUS, VIVIMUS maana yake kama tunaish basi tuendelee kuish,, hikii ni kilatini tuendelee kuish katika soka!

Leave a Comment