KIBURI CHA VAN GAAL NA UPENDO WA FALCAO

KIJIWE CHETU

KIBURI CHA VAN GAAL NA UPENDO WA FALCAO!

Waitalia wanakwambia Veritas vincit maana yake ukweli ni vita! Mwaka 2003 Real Sociedad ilibeba ubingwa wa la liga huku barcelona iliyokuwa chini ya Loius Van Gaal ikimaliza ya 12 nyuma ya point 20 kwa R Soicedad! Nakumbuka hiki kipindi ndicho alichomsajili Robert Enke (kipa), kiungo Gaizker Mendieta na kiungo mchezeshaji Juan Roman Requelme aliyesajiliwa kumrithi Rivaldo ambaye baada ya kuwa mchezaji bora (Ballon D' or) 1999 van gaal alimwambia rivaldo acheze winger ya kushoto lakin aligoma akitaka amchezeshe katikati matokeo yake van gaal alimwachia huru aondoke ingawa alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu

KUHUSU RIVALDO NA UBABE WA ROONEY
Rivaldo alipohojiwa alisema Van Gaal hakunipenda, ila cha ajabu niliachiwa huru nikajiunga Ac Milan ambapo niliweza kubeba UEFA! Van Gal alidai kuwa rivaldo alikuwa akiomba likizo ovyo, alikuwa mpenda pesa kuliko kujituma! Lakin najiuliza mimi binafsi inakuwaje kwa rooney huyu huyu aliyemgomea Moyes kucheze nyuma ya rvp lkn leo hii hata kipa naamin akiambiwa cheza basi atacheza!?

MAISHA YA FALCAO GIZANI
Huwa kuna kitu najiuliza kila siku, kwamba nani alimnunua Falcao? Kingine Je nan atatoa 45 kumnunua Falcao,? je nini shida ya falcao? Je falcao na van gaal wakiwa meza moja wanaangaliana vip? Kuna wakati mashabiki wengi wamekuwa wakimvamia sana falcao kwamba ameporomoka kiwango! Hebu tuangalie baadhi ya statistic zake,, amecheza mechi 14 amefunga magoli 4 na ku assist 6, tumwangalie di maria aliyesajiliwa E52 amecheza karibu game 19 amefunga magoli matatu ame assist 6,,, hivi mbona wengi wanamkimbilia falcao wanamwacha di maria?? Wapo watakaosema ni winga mwingine n mshambuliaji.. Lakin je n kweli di maria siku hizi ni winga? Je ni kweli falcao anacheza namba sahihi??

NINI TATIZO
Binafsi mimi simfikii van gaal kwenye utaalamu wa soka! Wala sijui mpira kumzidi.. Ila babu aliniambia mpira ni kuona! Hauna degree wala masters! Ukweli lazima usemwe.. Formation ya mipira mirefu 3-5-2 unaathiri kiwango cha wachezaji wengi mfano di maria ambaye n natural wing unampeleka katikati, rooney ambaye n foward mpka deep midfilder, falcao ambaye ni ST (striker) mpaka second striker! Mashabiki wengi wa united wanampenda sana falcao, kwa namna anavyocheza, patient yake, nidhamu uwanjan, records zake, na mchango wake lakin kiburi cha Van Gaal kitamfanya arudie yale yale ya rivaldo!...

IMANI YANGU KWA VAN GAAL
Statistic za van gaal na moyes hazijapishana sana ispokuwa tu nafasi! Hakuna jipya zaid ya mifumo ya ajabu ajabu kama gia za gari! Ukijaribu kuangalia statistic n kocha mzuri sana, ila kiburi kinachafua CV yake! Mpaka sasa amefungwa game 6 wakati moyes mpaka ligi inaisha alifungwa 12, man u hapo bado hajacheza na Tott, chelsea, arsenal, Man city n.k ambazo ushind n 50/50. Ni dhahiri kwamba van gaal hathamini nafasi ya falcao, naamin falcao n gentleman ila angekuwa ni kichaa mwingine basi dirisha dogo angeshaondoka! Injury ilimwathiri sawa lakin daah hali n mbaya maana amepiga mashuri 21 tu na di maria na rvp wamemzid dk 20 kila mechi walizoanza wote nikimaanisha amekuwa chambo kwenye sub! Niseme tu kama Waingereza KING CAN DO NO WRONG....niaamini kuwa van gaal hajakosea tusubiri ligi iishe tujue, kikubwa DUM SPIRO SPERO (as long as I breath) tutaona ipi mbivu na ipi mbovu.. Ila mshabiki mwenzangu wa United ni kwambie MACTE ANIMO (be strong)

No comments

Powered by Blogger.