MADRID WATAIMBAJE NYIMBO YA ROMA 2030

Kijiweni Kwetu

MADRID WATAIMBA VIPI NYIMBO YA ROMA YA 2030!

Waswahili husema lisemwalo lipo kama halipo basi laja! Naomba leo na mimi niwe mswahili maana ninalo lakusema kama halipo basi litakuja 2021 au 2030! Ukijaribu kuuliza watu 50 kuwa kwenye dirisha dogo la usajili ni timu gani imelamba dume basi watakwambia ni chelsea kumpata Cuadrado! Lakin kuna mtu hawa watu hamsini hawamjui! Ila naamin watamjua tu! Ana miaka 16 pekee yake! Wengi wanamwita messi ila sidhani kama mashabiki wa madrid watamwita "New Messi" wakati iker Casilas anapanda Ndege kuwelekea Madrid aliposajiliwa huyu mtoto ilikuwa hata bado hajazaliwa lakini leo hii wanacheza pamoja!

NI NANI HUYU
Amezaliwa Dramen Norway tarehe 12 dec 1998, n kiungo mshambuliaji hatari sana kwa umri wake kwa sasa! Sahau kuhusu Januzaj, ila wakati Gareth bale akiingia ile room yake special no126 kujiandaa kubadilisha nguo wakati wa mazoezi, muda huo huo ronaldo akiwa anapaki ferrari yake pale Ciudad Velebebas basi huyu mtoto huwa na watoto wenzake wa Castila chini ya Zinedine Zinade na mwanaye Enzo wakiwa kwenye chumba cha GYM Kilichotengenezwa na Bwana Carlos Lamela!kwa bahati fulan huyu mtoto atawaacha wenzake pale anaposikia sauti carlo ancelloti akiwaelekeza akina Ronaldo, yeye huenda kufanya nao mazoezi na timu ya wakubwa na kumwacha zidane akiwapeleka watoto wake la cantera wakapate msosi, ! Hapa namzungumzia mtoto wa mzee Hans Erick Odegaard ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji mkubwa huko norway

USICHOJUA KUHUSU ODEGAARD
Jina lake halisi huyu mtoto anaitwa Martin Odegaard amejiunga madrid kwa Ada ya Euro 2 lakini itaongekeza kutokana na kiwango chake! Analipwa euro 80,000 kwa wiki, kwa mbali naona kama anamzid hadi ivanovic akiwa na miaka 16 pekee! Aliichezea timu ya taifa akiwa na miaka 15 na siku 253 na kuwa mchezaji wa kwanza kuichezea timu ya taifa katika umri mdogo! Kabla hajajiunga na Madrid alikuwa mshabiki mkubwa wa Messi na aliweza kuweka baadhi ya posti twitter akimsifia sana Messi ila alipohamia Madrid alizifuta zote!

MAFANIKIO YAKE
Amecheza michezo mikubwa 25 na kufunga magoli matano! Pia ameichezea stromsgodset michezo 189 na kufunga magoli 41,na michezo 58 kwa magoli 15 kwenye michezo isiyo ya ushindani, amekuwa mchezaji mdogo kuwahi kucheza michuano ya kufuzu UEFA katika miaka 15 na siku 300, ameweza kuassist magoli 7 ya mechi 23 kwenye klabu yake hiyo! Aliweza kuvunja record ya kuwa mchezaji bora mdogo wa norway record iliyowekwa tokea mwaka 1910.

NYIMBO YA ROMA
Kwa maoni yangu nikimwona huyu mtoto hasa kwenye videos zake youtube basi namwona ronaldo mpya Kama sio Messi! Wakati ROMA anamwimbia mwanaye (ivan) 2030 basi madrid wanapaswa wamwimbie Odegaard 2030 ili afikie mafanikio yake! Ila cha kujiuliza Je atafanikiwa? Jibu ni ndio kutokana na umri na kipaji alichonacho! Hana lakupoteza kabisa, anajua mpira, ana umbo kama la messi, anacheza kama Messi, anajua kufunga, anajua chenga, mwepesi, anautumia vizuri mguu wa kushoto, yupo timu kubwa ambayo itampa motivation na promo! Hii nyimbo ya Roma ina umuhimu sana kwa Ordegaard ambaye ana mkataba wa mpaka 2021, mwanangu Odergaad kuwa uyaone mafanikio! ROMA anasema huwezi kuijenga Roma kwa siku moja, Odegaard anahitaji muda dunia imjue, hawezi kufanikiwa ghafla, ningekuwa na namba zake ningemtumia ile nyimbo whatsapp! Kama humjui hebu mwangalie Youtube halafu utajibu mwenye! Niseme tu Dum Vivimus, Vivimus (kama tunaishi basi tuendelee kuishi) tutamwona! Odegaard fortes fortuna iuvat ( bahati huenda penye bahati)

#dinho

No comments

Powered by Blogger.