DROO ZA UEFA

Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI itafanyika Ijumaa Machi 20 huko Nyon, Uswisi kuanzia Saa 8 Mchana, Bongo Taimu. Klabu 8 kutoka Nchi 5 za Ulaya zipo kwenye Droo hiyo ambayo tofauti na Raundi zilizopita, safari hii Droo hii ni huru na hivyo Klabu za Nchi moja hazibaguliwi na zinaweza kukutanishwa. Hivyo, safari hii upo uwezekano kuwepo kwa El Clasico ya Ulaya kwa Mahasimu Mabingwa Watetezi Real Madrid kupambanishwa na FC Barcelona. Mechi za Robo Fainali zitachezwa hapo Aprili 14 na 15 na Marudiano ni Aprili 21 na 22. Droo ya Nusu Fainali itafanyika Aprili 24 na Mechi zake kuchezwa Mei 5 na 6 na Marudiano ni Mei 12 na 13. Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI itachezwa hapoJumamosi Juni 6 huko Olympiastadion, Jinini Berlin, Ujerumani.

No comments

Powered by Blogger.