JE ENGLAND ITAINGIZA TIMU NGAP UEFA
Kijiwe chetu
VIGOGO EPL MBION KUTOSHIRIKI UEFA??
Ni Marufuku kwa Timu za England kupanda ndege au kucheza katikati ya wiki labda iwe kiporo au Fa, naomba warudie mabasi yao maana hakuna namna
MAN UTD, ARSENAL MCHECHETO
Baada ya fununu kusambaa sana ni wazi kwamba nafasi ya nne atakosa nafasi ya kucheza UEFA! Je ni arsenal? Je ni Man Utd? Je Southampton? Je ni Tottenhma?Je Ni vijogoo wa Anfield! Kama maneno haya yanaukweli basi ni wazi timu za England zitapita mbili halafu ya 3 kucheza play off (mtoano) vita itahamia kwenye Top Three na sio Top Four maana nafasi ya 4 haitakuwa na faida kwa Van Gaal na itakuwa kwa Mara ya kwanza Arsenal kukosa UeFa chini ya arsene Wenger
MARUFUKU KUPANDA NDEGE
Baada ya mechi ya chelsea nilikuwa na marafiki zangu fulani hivi ambao pia ni mashabiki wa EPL nikawaambia kuwa kama chelsea ametoka basi ni marufuku kwa timu yoyote England kupanda ndege! Nikimaanisha kwamba zote zimetoka zitarudia mabasi yao kama kawaida, maana hawatakuwa tena na michezo nje ya England, fununu nyingi ambazo zimeenea sana hapa mjini hasa kipindi hiki ambacho timu za England zimeharibu kwenye michuano ya UEFA! Kwamba msimu ujayo England Itapeleka Timu 3 tu!
HIZI NI FUNUNU TU
Baada ya fununu hizi kuwanyima usingizi mashabiki wengi basi nataka niwaondoe wasiwasi huo kabisa ndugu zangu wa Emirates na wale Wa Old trafford! Hakuna kitu kama hicho! Katika mashindano ya UEFA kuna makundi Matano, kundi la kwanza ni kuanzia nchi Ranki namba 1-3 ambazo hupeleka timu 4, kundi la pili ni kuanzia Ranki ya 4-6 hizi zinapeleka timu 3! Kundi la 3 ni ranki namba 6-15 hizi nchi zinapeleka timu 2! Kundi la 4 ni ranki ya 16-54 (kutoa Liechtenstein) hizi nchi zinapeleka timu moja tu, na kundi la Mwisho ni Mshindi wa UEFA NA UROPA LIGI (wote wanapata nafasi ya kuingia free)jl
MABADILIKO YA UEFA MWAKA 2015/16
Kamati ya Uefa Iliyokaa May 2013 ilifanya baadhi ya Mabadiliko ambayo yataanza Mwaka 2015 kuendelea mpaka 2018, mabadiliko haya ni kama yafuatayo! Mshindi wa Uropa Liga atapata nafasi ya kuingia ila kwa Play off, pia kuna ongezeko kutoka timu 4 mpaka 5, (kama mshindi wa UeFa au UroPa anatoka nchi fulani kati ya ranki ya 1-3 lakini yupo nje ya Top Four basi nchi hiyo itapeleka timu 5 ina maana timu 4 za mwanzo zitapita kama kawaida na mshindi wa Uefa nae atapita bila tatizo! Lakini kama mshindi wa Uefa na UroPa zinatoka nchi moja Basi nafasi ya 4 itachukuliwa na mshindi wa UroPa na Nchi hiyo itapeleka timu 5 pekee yaan 3 za juu, mshindi wa uefa na mshindi wa Uropa atachukua nafasi ya anayeshikia nafasi ya 4!
JE ENGLAND ITAPELEKA TIMU NGAP?
Kwa maaelezo hayo mafupi ingawa yanachanganya kwa kiasi fulani basi hizi ndizo sababu za England kupeleka timu 4!
Sheria (ranki za uefa)
England ni mojawapo ya nchi ambazo zinaruhusiwa kupeleka timu 4 yaan kundi lakwanza ambalo lina ranki ya 1-3! Ranki ya kwanza kabisa ni uhispania ambayo ina Point 97.713 na inaruhusiwa kupeleka timu 4, ranki ya pili ni England ambayo ina pointi 84.748 inaruhusiwa kupeleka timu 4, na ya 3 ni German ina pointi 81.641 na inaruhusiwa kupeleka timu 4! Kwa mantiki hiyo ligi ya Uingereza haitaathiriwa na chochote itaendelea kupeleka timu 4 kutokana na ubora wake na haiwezi kuporomoka kirahisi mpaka kundi la pili ambalo linajumuisha Italia, ureno na Ufaransa!
Sababu ya Pili ni Uchumi!
Uefa inapata pato lake kutokana na Mechi na Matangazo! Kwa mfano huwa wanaangalia ligi ambayo ina ushindan mkubwa ili kuweza kulinda pato lao! Kwa mfano huwezi kupunguza timu za England ambazo zinaingiza Pato kubwa halafu unaipeleka timu ya Serbia ambayo uwanja wao hauingiizi hata mashabiki 30,000 unaizitoa timu ambazo zinaingiza biashara kubwa kutokana na viwanja matangazo na mauzo ya jezi n.k. Kukosekana kwa timu kama Man utd, Ac Milan, Inter Milan huwa kunaleta changamoto kwenye suala la Mapato! Unakuta timu zilizoingia hazina msaada mkubwa kwa Uefa kama hizo timu kubwa!
Sababu ya mwisho ni kwamba.. ubora wa uefa unaporomoka endapo tim itakuw na matokeo mabovu kwa misim mitano ndo inapunguziwa idadi ya timu kuingia uefa
KWAHIYO MUWE NA AMANI KABISA! INGAWA NI AIBU KUBWA SANA IMEPITA ENGLAND NA NI WAZI KWAMBA HUENDA ENGLAND IKAWA LIGI SAWA NA LIGI NYINGINE LAKIN UMWAGAJI WA PESA NA MATANGAZO UNAIFANYA LIGI CHIPSI (YAAN LIGI PENDWA) KWA SABABU TAZAMA WOTE WAMETOLEWA NYUMBAN,

Leave a Comment