MZARAMO ALIYEFANIKIWA ULAYA
Kijiwe chetu
MZARAMO ALIYEFANIKIWA ULAYA
Ukitaka kujua kama kuna watu wenye maneno basi watafute wazaramo au wazanzibar! Hawa watu wanamaneno mengi na hata ukikaa nao basi huwachoki maana wanajua kutengeneza maneno yaume au yalize au yachekeshe
Leo tusafiri mpaka mji wa Lisbon ureno maeneo ya Setubal huku tunakutana na baba wa watoto Matilde (msichana) na Jose Jr aliyewazaa na mkewe kwa Jina Tami! Wazungu wanasema kuwa ana lafudhi ya kimediterania ila mm namwona kama ana lafudhi ya kizaramo! Tuachane na hayo!... Duniani kuna makocha wengi sana lakini ndani yao kuna mameneja na waalimu! Mpaka sasa nmeona waalimu watatu pekee pale ulaya wenye mafanikio ( sir Alex Ferguson, Proff Arsen Wenger na Frank Rijkaard) ila mameneja nmeona akina Jose Mourinho, Pep Guardiola wao hutegemea zaidi Pesa kutengeneza timu kuliko kuibua vipaji!
******
Mfano Guardiola aliondoka Barca alipotaka timu iuze baadhi ya wachezaji inunue wapya wakagoma! Pia kwenye makocha kuna mainjinia kama diego Simeon, Raphael Benitez, Carlo Ancellot, weka pemben marcello Lippi yupo Mzee Jock Stein ambae kwa kiasi fulan anamkaribia fergie kimafanikio! Natoa Pongezi kwa mashabiki wa chelsea hususani Mourinho kwa kushinda kikombe cha FA
KWANINI NAMUITA MZARAMO!
Huwa mimi napenda sana kumsikiliza Mourinho hasa anapokutana na waandish wa habari! Ana majibu ya ghafla ambayo huwezi kutarijia! Kwa kipindi cha hivi karibuni amekuwa na vita na marefa kwa kile alichodai kuwa kuna kampeni za kumshusha! Kwa mfano alimvamia kwa maneno makali sana refaree Atkinson kwenye mechi dhidi ya Burnley akidai kuwa kadi nyekundu ya Matic haikuwa halali, kwenye game ya soton akadai tena Fabregas alipaswa kupewa penati, akalalamikia kitendo FA kumsimamisha Costa kwa kumkanyaga Emre Can! Ila naamin nyani haoni kundule kwa mfano, alichofanya Ivanovic kwa McCathy alistahili kadi nyekundu, alichofanya Garry Cahil kwa kane lilikuwa wazi, alichofanya Cahill kwa Sanchez Pia hilo hajaliona!
Majibu yake
Amekuwa ni kocha mwenye maneno Mengi sana! Kwa mfano nakumbuka aliwahi kuuliza kwanini unakuwa na Presha sana uwanjan akajibu "preshaa???? Presha ya nini?? Presha ni kwa watu million 100 waliokosa vyakula kwa ajili ya watoto sio kwenye Mpira! Akaulizwa tena kwanini unaigopa Barcelona na matumizi ya kuweka ukuta (kupaki basi) akajibu kwenye kamusi yangu ya mpira hakuna neno woga! Mimi sio mwoga wala sina uoga!
NI MWANAFUNZI ANAEPIGA WAALIMU WAKE!
Ukijaribu kuangalia vizuri Jose Mourinho amekuwa kocha mkuu kwa kipindi cha miaka 12! Huyu jamaa alikuwa Mwanafunzi wa Bobby Robson ambaye alifanya nae kazi Sporting CP, Porto na Barcelona akiwa kama kocha Msaidizi baadae akaja mwalimu mwingine loius Van Gaal Pale pale Barcelona! Kuna wakati Van Gaal alimwacha mourinho afundishe kikosi cha kwanza na aliweza kubeba Copa Catalunya 2000!
AMEPIGA VIP WAALIMU WAKE
Amecheza karibu mechi 727 ameshinda tuzo 21 kila tuzo baada ya mechi 34.6, wakati mwalimu wake Van Gaal amecheza Mechi 831 tuzo 19 kila tuzo baada ya 43.73! Huku Mwalimu mkuu Sir Bobby Robson akicheza Michezo 1446 tuzo 13 kila tuzo 111.23! Wakati mwalimu wa Jiran Arsen Wenger akitumia mechi 1487 na tuzo 17 kila baada ya mechi 87.47! Bado tu haitoshi??? Waziri wa Wizara ya Elimu sir Alex Ferguson ilibidi atumie Michezo 2131 kupata tuzo 44 kila baada ya mechi 48.43!
Kama hilo halitoshi
Ametumia miaka 12 kubeba tuzo 23, wakati, anceloti amekaa miaka 20 na kupata tuzo 17, ferguson miaka 28 na kupata 38, Wenger miaka 26 tuzo 17, Van Gaal miaka 23 tuzo 19! Hujaridhika bado?? Twende mbele turudi nyuma Jose Mourinho Mbali na kutpendwa na Mashabiki wengi wa timu pinzani
basi huyu ni koboko ya waalimu au tuangalia uso kwa uso dhidi yake na Kocha mkubwa kuliko wote duniani sir Alex Ferguson, wamekutana michezo 16, mourinho ameshinda 6, droo 7,na kupoteza 2, kumbuka akiwa na Porto alipata droo pale old trafford, na kushinda kule porto marudiano mnamo mwaka 2004, akiwa kama kocha wa chelsea ameshinda michezo minne, amedroo 4 na kupoteza moja tu! Akiwa na inter alidroo moja na kufungwa moja mwaka 2009, akiwa Madrid alishinda moja pale Old trafford na Droo pale Bernabeu! Umeona mwanafunzi anavyopiga waalimu wake!
HUYO NDO JOSE MARIO DOS SANTOS MOUR FELIX... hahahah haitwi Mourinho!??? Ana miaka 52 tu bado ana mafanikio makubwa!
Leave a Comment