POLENI AZAM BADO MUDA UPO
Kijiwe chetu
PESA HAINUNUI MAFANIKIO
Kama ningekuwa msomi maarufu anaekubalika Dunian basi ningeondoa Somo la Hesabu kabisa maana hili somo ndilo linal ofanya watu wengi wanafeli. Kama hilo halitoshi niliwahi kuambiwa na Mwalimu wa aCademy kuwa mpira ni mahesabu! Kama mpira ni mahesabu basi Azam wamepata F kama sio D!
MASWALI YA HESABU YA KUJIULIZA
Wakati taarifa za chini chini zikiendelea kuhusu kutimuliwa kwa kocha wao mkuu mimi ninakuwa na maswali mengi ya kujiuliza?inakuwaje AZAM inatolewa mapema ktk mechi za kimataifa? Ni ubovu wa ligi yetu? Ni mfumo mbaya wa soka letu? Au hatupati bingwa sahihi kwny ligi yetu (matokeo ya kununua) ndo maana klabu zetu hazifurukuti mechi za kimataifa? Kwa nn tusirudi nyuma na kujiuliza Simba walipitia njia zipi miaka ile wkt ipo chini ya ufadhili wa Azim Au ahadi ya zawadi ya magari ya Chai Maharage ndo ziliwapa hamasa?kikosi cha Simba kilikuwa na Mtu malota! Je malota si yupo hai?? Kwanini asiulizwe walifanya nini!!!
ADA KUBWA NA MATOKEO MABOVU
Watoto wengi wa matajiri hawapendi kusoma, hata watoto wa Mzee Bakhresa (Azam) wamekataa shule wamepigwa tatu na el merrekh! Kufikia mwaka 2014 azamu ilikuwa na wachezaji wa5 wanaolipwa zaid ya milion 2! Wakati allan Wanga anatokea Fc Leopard kwa 10m kujiunga na El Merrekh huku akilipwa million 5 kwa mwezi Azam wao wana kipre tcheche, Kipre balou, Aggrey Morris, brian Umonyi, hawa wote ni million 4 hivi, kulikuwa na taarifa kuwa mshahara wa mchezaji wa kikosi cha kwanza azam sio chin ya Million moja! Sasa najiuliza Azam wanataka nn??
MAANDALIZI YETU SIO MAZURI
Ninachokiamini Kama mtoto wa kiume kama kumaliza sahani moja ya uji nyumbani kwenu ni shida basi usitegemee kumaliza beseni la mihogo ukweni.. Azam kinachowakwamisha ni ligi yetu ya bongo ambayo binafsi naiona kama uji! Hakuna ushindani mkubwa! Timu zipo 2 ngumu tu weka pembeni mbeya city! Kwa mantiki hiyo azam wao hujiandaa kunywa uji kwa wingi lakin inapotokea mihogo wanambwela! Kama tunataka kufanikiwa Kimataifa kwanza tuijenge ligi yetu iwe ya kiushindan! Maana hata mkiweka Pesa nyingi kiasi gani mtaishia kuwa Anzi makhachkala tu!
PESA HANINUI MAFANIKIO
Kwanza hebu jiulize sir Alex aferguson aliposema PESA HAINUNUI MAFANIKIO unahisi alikosea?? Wengi waliona kama n majungu kwa Man city lakin tuchukulie mfano Mwepesi PsG, Man cty, Monaco na wengine wengi Wanalipi jipya Barani ulaya!? Kama Mpira n Pesa Mbona Marekani nchi tajiri dunian haina ligi bora kama za ulaya??? Hili n funzo kwa Azam wasitegemee sana kwenye umwagaji wa Pesa wakasahau juhudi!! Pesa huaandaa mafanikio na Juhudi hukamilisha maandalizi hayo! Kama Mpira ni Pesa basi tuchukue mshahara wa Ronaldo E600000 kwa wiki tumpe welbeck tuone kama atafikia nusu ya uwezo wa Neymar Jr. Angalia thaman ya kikosi cha Atletico Madrid??? Angalia thaman ya kikosi cha Bretford kilichoifunga Chelsea 4.. Angalia thamani ya kikosi cha MK DONS kilichompiga Man united 4!
PESA HUANDAA MAFANIKIO
Ninachoamini mimi n regional balance Kwenye soka! Kuwe na ngome zaid ya 4 zenye ushindani kisoka! magharibi (mwanza) kusini (mbeya) kaskazini (arusha/moshi) mashariki (Dsm). Namaanisha uwekezaji usiegemee upande mmoja tu! Hii huleta pia chachu ya ushindan kwa ligi za ridhaa (kimkoa, kiwilaya n.k) kama ikitokea katika pande zote hizi zipo klabu kubwa na zenye Pesa basi hata ushindan unakua kwa kasi, hivyo timu zinakuwa zimekomaa kikamilifu hata kimataifa! Uwekezaji usiegemee Dar Pekee yake! Wapo watu natamani wafike mahali fulani Kama Panone Ya kaskazin, mbea city, Madini ya Arusha, stand n.k. Hili huleta changamoto na zile timu kubwa za dar zitaweka juhudi kubwa. Maana leo hii Simba ikija arusha kucheza na JKT oljoro inakuja kujichulia Ponti na sio kushindana, Binslum kwanini mmeiacha coastal Union!??!
TUJIFUNZE KUPITIA AZAM! AZAM BADO WANA NAFASI YA KUFANYA MAKUBWA TUSIISHIE KUWAKATISHA TAMAA PEKEE!
Leave a Comment