MOURINHO ALIIBIA MTIHAN

MOURINHO ALIIBIA MTIHANI

Waswahili wanakwambia hakuna jipya chini ya jua, kila utakachokifanya wewe jua kilishafanywa wewe unafanya marudio tu.

Kuna watu wabunifu sana hapa duniani, mwaka 1930 kuna kitu ndugu Karl Rappan alikitambulisha kule uswis kinajulikana kama Catenaccio. Hii Catenaccio ilianza kuwa Maarufu miaka ya 1960, inter Millan ndio klabu pekee iliyofanikiwa na huu mtindo miaka ile. Mwaka 2010 Jose Mourinho alitumia mfumo huu akiwa na inter dhidi ya Barcelona kwenye Michuano ya UEFA! Kumbe Mou alichungulia mfumo huu uliotumika Miake ile. Kwa sasa mtindo huu unaitwa Kupaki basi, kuzuia zaid kuliko kushambulia. Mwaka ule inter walikuwa na Mtu Kama Guameri, Burgnich, Facchett, jair, tagnin halafu katikati mwanaume luis suarez akimaliza kazi, mbele alisimama Milani tu.

MTINDO UNAOBOA ZAIDI
Ukiangalia mwaka 2010, Mourinho alikuwa na watu kama Pandev, zannetti, chivu, na vichaa wengine waliomchafua Roho lionel Messi,Mourinho alimchungulia Helenio Herrera ambaye ni mwarijentina aliyefanya mfumo huu wa Rappan kuwika zaidi miaka ile ya 60. Karl Rapan alitumia aina hii ukijengwa na beki mmoja kisoka tunamwwita Verroullier ambaye huyu anakaa mbele kidogo tu ya kipa, waitalia wanamwita LIBERO england wanamwita Sweeper bongo tunamwita Mkoba! Kazi yake ni kuchafua na kuosha tu. Hapa unakutana na kitu kinaitwa Man to man kama chivu na messi, mtu hatembei labda wakati wa kunywa maji tu. Watu wengi hawapendi mtindo huu maana unatoa ladha ya mpira ndio maana Mourinho hapendwi.

HUU MFUMO UPOJE
Mfumo unakuwa hivi 1-4-4-1, yaan nyuma ya mabeki wanne wanaweka beki mwingine,mourinho amekuwa kipenzi cha mfumo huu, mfumo huu unahitaji wanaume wa shoka, unahitaji akina Michael Essien, akina obi mikel, akina Pepe, na wengineo Wengi, miaka ile kocha wa Nereo Rocco alifanya maajabu Serie A baada ya kuipeleka Triestina nafasi ya pili, mfumo huu kwa sasa wanatumia watu kama Stocke City, Sunderland na Mzee Ancellot aliwahi kuutumia sana. Cesar Prandell aliutumia kwenye Michuano ya Uefa 2012, pia kocha Mwingine wa kiitalia Cesare Maldini aliwahi kuupenda sana mfumo huu ukiachila mbali Giovan Trapatton ingawa hawakufanikiwa sana kama alivyofanikiwa Jose Mourinho ambaye aliwachungulia wenzake akafaulu. Mwingine aliyefanikiwa ni Dino Zoff mwaka 2000 walipofika fainali ya Euro ambapo Italia walifungwa kwa Goli la Dhahabu na ufaransa!

KUPOROMOKA KWAKE
Kuanzia miaka ya 1980 huu mfumo uliporomoka baada ya mfumo wa 4-2-4 na mtindo wa total football kukua kwa kiasi kikubwa! Kwa mfano timu ya taifa ya italia ilianza kutumia mfumo huu, mwanzon Pointi za mchezo ilikuwa ni mbili kwa msindi, mojaa kwa droo, zero kwa anayefungwa, lakini baada ya kuongezeka mpaka point 3 basi timu zilipata moyo na kuanza kutumia mfumo wa kushambulia zaid ili kupata ushindi wa point tatu ambazo ni nying ukilinganisha na Mwanzo, pia mfumo huu ulichokwa maana hakukuwa na mvuto wala soka safi, kilichoboa zaidi ni pale Inter ilipopigwa 2 na ajax fainal na Ac millan kukungutwa 6 dhidi ya ajax zote kwenye fainali ya Uropa hapa ndipo catenaccio ikayumba.

Mfumo huu unafaida zake pia, kwanza kumpoteza kabisa namba 9, kupunguza idadi ya magoli, na pia kufanya timu pinzani ichoke na kujisahau maana muda mwingi timu pinzani inakuwa na Mpira, kama mchezo wa chelsea na Barca ambapo Tores alifunga goli la kushtukiza!,huu mfumo hauhitaji kipaji, ufundi, udambwidambwi wala nn zaidi kuanua mipira, kukaba na kuzuia. Mfumo huu ndio chanzo cha kutokea mabeki bora dunian, kama Paolo maldini, Gaetana Sceria, Alessandro Costacurta, na Claudio Gentile ambapo wengi wao walikuwa walatin. Mfumo huu uliipa chelsea ubingwa chini ya Di matteo, inter Ubingwa wa uefa chini ya Mourinho, uliipa inter Ubingwa wa ligi mara 3 miaka ile, na uefa mara mbili chini ya Helenio Herrera ambaye baadae alihama Inter akaenda Roma akatumia mfumo ule ule na akashinda ubingwa wa ligi.

No comments

Powered by Blogger.