EBOLA ISIYOTIBIKA YAZUKA ULAYA

EBOLA ISIYOTIBIKA YAZUKA ULAYA!

Hivi ulishawahi kuwaza ikitokea siku Fredrick Sumaye, Edward lowassa, na Rostam waunde chama chao halafu waingie kwenye uchaguzi mkuu kushindana na chadema na Ccm?? N kiumbe gani atainua shingo yake kushindana na huu utatu??? Usiombe ikatokea!

Kwa wale waliobahatika kuona mpira wa vibukta vifupi achana na huu wa akina Julio Cesar wanavaa mlegezo nazungumzia ule wa juzi juzi tu hapo sio mbali sana, akina Romario, Michael Laudrup na Hristo Stoichkov? Halafu jiwe la msingi lilikuwa kwa Pep Guardiola, Ronald koeman, na Juan Carlos?? Benchi akiwa Bwa Johan Cruyff! Baadae kidogo wakatokea wanyama watatu Ronaldinho, Deco na Samuel eto'o, hawakutosheka ikaja Samuel eto'o, thiery henry na Lionel mess hii ndo iliyomfumua Madrid 6-2 2009 pale pale bernabeu hawa wanyama mwaka ule walifunga magoli 100 wote henry 26, Eto'o 36 na messi 38! Ilibidi aletwe David villa, ili akae na Messi, na Pedro kuziba mapengo ya eto'o na herny, wakafunga magoli 98 messi 53, villa 23 na pedro 21 tena wakamtandika Man utd pale pale sebulen kwao Wembley

Rafiki yangu mmoja mshabiki wa Man cty aliniambia hakuna usajili wa Presha uliowahi kufanyika dunian kama wa bale! Nikamuuliza kwanni? Akanijibu kuwa baada ya Barcelona kutikisa na mfumo huu wa false 9 yaan wachezaji watatu mbele nao wakatamani wawe na kitu kama hicho! Lakin target yao kubwa ni Neymar, ila kwa bahati mbaya walimkosa! Na wakatumia pesa nyingi kutokana na wenge, Presha na woga wakajikuta wamempigia Magoti Redknapp, Redknapp akawapiga za uso basi wakatoa 86 ili wapambane na Messi, iniesta na Neymar. Madrid wakatengeneza kamfumo kao wakakaita BBC, kweli kalifanya kazi kwa namna fulan.

EBOLA ISIYOTIBIKA
Zaman watu walikuwa wakiOmba wakutane na Trio yoyote dunian ilasio ya Ronaldo, Rivaldo na Ronaldinho (brazil), lakini hii ilishapita, imekuja nyingine, Messi, Neymar na Suarez! Msimu huu wameshafunga magoli 105 kati ya mechi 132 tena suarez alikuwa nje miezi miwili bila kusahau kuwa Messi alikuwa nje ya fomu hapo jumlisha magoli ya Leicester city, hully city, burnley, Qpr na suneelrndan ndo wanafikia hiyo idadi, wote wametengeneza magoli 51. Hizi assist uingereza hata ujumlishe Assist zote nadhan hawapishani sn. Messi amecheza mechi 50 amefunga 53 na ameasst 27, Luis Amecheza 39 amefunga 21 na ameassist 18, Neymar amecheza 44, magoli 32 na assist 6. Hiyo ndio ebola ambayo ikikupata basi sijui utapona vipi!

Madrid nao
Msimu huu madrid imemkosa sana luka modric lakin kazi ya james Rodriguez inanifanya nimsahau. Hii trio ya Ronaldo, bale na James binafsi naona ndo nzuri kuliko BBC. James au mwalimu wa hesabu amekuwa chachu ya ushindi kuliko Benzema! Tatizo kubwa hapa Madrid ni uchoyo na umimi. Kuna wakati bale hampi pasi Cr7, kuna wakati benzema akipewa ana ng'ang'ania kufunga, Isco ndo kabisaaa anatoa pasi akizidiwa. Wengi hapa wanashindana na Ronaldo. Ronaldo amegoma kupokea majukumu ya Messi ya kutoka kwenye box aje atengeneze. Ni kweli ronaldo umri umeenda anakwepa sana Majeruhi ndio maana inakuwa uamuz mgumu kwake kuja pemben au katikati kutengeneza mashambulizi zaid.

Nikukumbushe tu.
Huu ugonjwa uliwahi kuzuka pia miaka ya nyuma, Xav mess na iniesta, pale Man utd ulikuwepo Ronaldo, Rooney na Tevez, juventus ulikuwa Del Peiro, Vialli na Ravanelli, ac milan Alikuwepo rijkaard, Van Basten,na Gullit, miaka ya 80 walikuja akina Maradona, Giordano na Cereca pale Napoli, miaka 15 kabla sijazaliwa miaka ya 1977 mpaka 1985 pale Anfield walikuepo Hansen, Sounes na Dalglis mabeki hapa walikuwa Alan,na Captain Graeme katikati ya dimba nadhani kumwembe anawakumbuka, hapo Ajax sasa alikuwepo Cruyff na rep. Miaka ile ya akina mtume old trafford walikuwa miamba ya soka Best, law na charlton waliitwa THE HOLLY TRINITY. Charlon pekee ndiye aliponea ajali ya Munich. Walishinda kama wachezaji bora wa ulaya best 1968, law 1964, charlton 1966. EPUKA EBOLA

No comments

Powered by Blogger.