MARC VIVIAN FOE HAKUFA
kijiweni kwetu
MARC VIVIAN FOE HAKUFA
Kankava alimshtukia na alimkimbilia na kumnyanyanga Gusev ulimi wake uliokuwa ukielekea kwenye koo! Ni wazi kwamba kama angeumeza basi Gusev angepoteza maisha! Najiuliza ingekuwa mchezaji mwingine kama pepe huenda angemtukana Gusev kwamba kajiangusha
*################
Wakati namwona Piermario Morosin mnamo tar 14/04/2012 akipiga magoti nakushindwa kusimama, alijitahid kusimama alijiinua alianguka tena chini mwenyewe, nadhan ile ilikuwa siku yake ya mwisho kusimamia miguu yake maana baada ya kuanguka hakusimama tena binafsi nilijisikia vibaya sana, niliumia sana kwa yule kaka kupoteza maisha yake kazin, uwanja mzima ulipigwa na butwa!
GUSEV AKUTANA NA ISRAEL
mwaka jana Jaba kankava alifanya jambo ambalo dunia nzima, Dynamo kievs, dnipro na familia ya Oleg Gusev hazitokaa zimsahaua, hata ule ushindi wa hii darby haukuwa na maana kama alichofanya Kankava, Gusev(nahodha) wa kiev aligongana na kipa wa Denys Boyko na alipoaanguka Kankava alimshtukia na alimkimbilia na kumnyanyanga Gusev ulimi wake uliokuwa ukielekea kwenye koo! Ni wazi kwamba kama angeumeza basi Gusev angepoteza maisha! Najiuliza ingekuwa mchezaji mwingine kama pepe huenda angemtukana Gusev kwamba kajiangusha lakini Kankava aliondoa upinzani akamkimbilia akaingiza mkono mdomon na kumtoa ule ulimi la sivyo basi tungesema mengine!
++++++++++++++++++++++++
Tar 26/06/2003 ni mwaka ambao dunia nzima, na wakameroon hawatousahau kamwe! Marc vivian Foe, baada ya kushuhudia Goli la Pius ndiefu akiifunga Colombia, bila shaka hili lilikuwa goli la mwisho kwa Foe kuliona, baadae dakika ya 23 refaree Markus Merk wa ujeruman alimpatia kadi ya njano Foe pia hii ilikuwa kadi ya Mwisho kwa Foe! Ilipofika dakika ya 72 alianguka mwenyewe na ghafla alipoanguka alibadilisha macho na kuanza kupumua kwa nguvu, wakati Kankava akitumia dakika takriban 5 kumuokoa Gusev hapa madaktari walitumia dakika 45 kumuokoa Foe, najiuliza kwanini hakutokea kankava mwengine kuokoa maisha ya Foe?
Foe aliishi dakika 45 pekee akiwa amekufa! Yaan zile dakika 45 alizokuwa akiokolewa aliishi akiwa amekufa! Kuna kitu najiuliza sana kwenye hii dunia, Foe alifanya nini? Man cty wameifuta jezi 23 aliyokuwa akivaa pia wameweka jiwe lenye jina lake palepale uwanjani, Louvre-lens klabu yake ya zaman imetenga eneo la uwanja lenye jina lake pia wameifuta jezi namba 17, swali linanijia hasa napoyaona machozi ya thiery Henry huku akinyoosha mkono juu kumkumbuka Foe, kwanini Foe anakumbukwa namna hii? Je aliwahi kuwa mchezaji bora wa dunia? Je aliipa Cameroon world Cup? Amefanya makubwa mangap?? Mpaka sasa wachezaji takriban 122 wamepoteza maisha yao uwanjan tokea mwaka 1889 Willium Cropper mpaka leo mimi namjua Foe tu, Di jones aliichezea man cty na alikufa uwanjan lakin hatujui! Binafsi nakubali Upendo wa Foe uliiteka dunia, kubali ukatae Foe alipendwa zaid na atazidi kupendwa na kukumbukwa, sio kwa kukaba, sio kwa nguvu aliyonayo, sio kwa pasi ila tu alikuwa na nyota ya pilau uzaramon, ndio maana Wakameroon wanakwambia simba hafi analala, Foe ni simba alyelala tu! *********
NAWATAKIA UPENDO ZAID TIMU YOTE YA SOKA ILIYOPO MBINGUN, NAAMIN HUKO MBINGUN BADO FOE ANAZIDI KUPAMBANA KUTUOMBEA! SIMBA WA PEKEE WA DUNIA! MBELE YETU NYUMA YAKE
#dinho
Leave a Comment