PEREZ INATOSHA BABU

PEREZ NKURUNZINZA MWEUPE

Unapokaa Meza ya walevi, hata ukiwatukana vipi hawatakujibi endapo
utamwaga vinywaji mezani.. Mwaga pesa maovu yako yataonekana Mema!

Waliondoka akina Angel Di Maria, Xabi alonso, na Mesut Ozil. Istoshe
wamemtoa Moratta wamemwacha benzema! Cha ajabu Morrata kawaliza!
Ninapoyaangalia mafanikio ya Real Madrid kwa miaka 6 mpaka 12
yametokana na Pesa na sio Uongoz bora! Jiulize tu ujio wa akina de
lima, akina figo na wengine, achana na kuondoka kwa makelele ambako
kulizua utata sana! Alimpomfukuza Del Bosque msimu wa 2004 miez minne
iliyofuata ilipoteza Copa De larey, iliondolewa Uefa na Monaco na
ilifungwa mechi 6 kati ya saba mfululizo la liga na Valencia akatwa
ubingwa


Wakati makelele anaondoka baada ya ugomvi na Perez, aliletwa David
beckham wengi walisema ni sawa na kupaka rangi ya dhahabu kwenye gari
lenye injini mbovu. Makelele alikuwa ndiye mchezaji tegemezi lakini
alikuwa kwenye listi ya wachezaji wanaolipwa mshahara mdogo! Alipotaka
mshahara mkubwa Perez aligoma na kumuuza chelsea. Mnamo mwaka 2003 huu
ulikuwa mwaka wa Galactico chini Vicente Del Bosque, pamoja na kutwa
ubingwa wa la liga bado Perez alimtimua tena kwa kashfa nyingi akisema
"hakuwa mtu sahihi kwetu, alikuwa sio kocha wa matgemeo yajayo,



Mnamo tar 23 june 2003 wakati wa sherehe za kombe lao la 29 la laliga
picha mbalimbali zilisambaa mtandaoni zikionesha wachezaji kama iker,
morientes, Guti, hiero, na wengine wakipigwa na butwaa wakati Perez
akiwahutubia Madridistas kuhusu kutimuliwa kwa Del Bosque. Mwaka 2007
alisema maneno ya kashfa sana kwake, "anaenda kuifundisha Spain? Kwa
lipi?? Hana sifa za kufundisha! Ni mbovu, lakin del Bosque atabaki
kuwa kocha wa kukumbukwa vizazi vyote hispania ispokuwa yeye mwenyewe
Perez.
Msimu uliopita Ancelloti amebeba UeFa, Super Cup, world Cup club, na
copa de la rey, lakin cha ajabu msimu huu ametimuliwa! Sasa sijui
anamtaka nan? Skuona sababu ya ancellot kutimuliwa! Msimu kwenda
vibaya haimaanish kuwa hafai!

Matus yake
Alipomchukua beckham alisema, Makelele hawezi kupiga mpira hata mita
3. Kwa mantiki hiyo alimleta Beckham ili apige hata zaid ya mita kumi
huku akisahau kuwa Beckham sio kiungo mkabaji. Juzi juzi alimtoa Xabi
alonso akamleta Kroos aje acheze namba 6! Nadhan wengi waliona namna
madrid walivyopotea katikati! Alipomtoa Di maria alimleta james cha
ajabu james sio kiungo wa pemben ila wa kati! Alipomtoa ozil alimleta
isco ila mpaka sasa isco hajafikia hata Robo ya pasi alizopiga Mesut
Ozil. Timu kwa sasa inacheza nje ya mfumo, hasa modric, na kroos! Kwa
mfano ilipata point 3 tu kati ya 12 dhidi ya Barca na Atletico
ikashindwa kuwafunga wazee wa turin.Lilitokea juzi juzi, Wachezaji
wote wa madrid wamekerwa na kitendo cha Ancellot kutimuliwa!
Walichezaji walifurahia ukufunzi wake! Kati ya Makocha 46
walioifundisha madrid kwa miaka 113 huyu anaweza kuwa na mafanikio
makubwa na asilimia kubwa za ushindi.

Istoshe
Mwaka 2012 alifanya kituko cha aina yake kwa kudai kwamba eti ukitaka
kugombea urais shart uwe mwanachama kwa takriban miaka 15-20,  na
lazima uweke million 83 kama garantii amabayo ni sawa na 15% ya budget
ya madrid. Hayo ni maajabu maana hakuna tajiri wa kihispania mwenye
uwezo huo, kwa mfano mwaka 2013 ilibid mtu atoe 120 milion agombee
urais! Lakin Calderon ambay mwaka 2006 alikuwa rais wa Madrid
alimnafikia kuwa "ili ahakikishe ana kuwa nkurunzinza basi mgombea
lazima awe na jina linaloanza na heruf F-L-O" ukiachana na na 2003
alikaa miaka 9 huku akifukuza makocha 8.


MIUJIZA YAKE
Wakati anaichukua madrid mwaka 2000 aliwashangaza wengi baada ya
kumnunua mchezaji na kepten wa Barca luis Figo! Mwaka uliofuata
alimchukua Zinedine zidane baada akamleta De lima. Isistoshe alimleta
posh baby David beckham, Ronaldo christiano na wengineo wengii sana

No comments

Powered by Blogger.