SIMULIZI YA SGURD SEHEMU YA KWANZA
SEHEMU YA KWANZA
walipokuwa
maeneo ya tabata mawenzi, wasijue na cha kufanya
wakiwa
wamechoka kwa safari yao ya mizunguko, haruna alionekana
kulegea
sana kutokana na njaa, akamwomba rafik yake wapumzike angalau kidogo,
mussa
alikataa akamsihi waendele mbele huenda Mungu akasikiliza sala zao,
mbele
kidogo walikutana na Yoshua waliesoma nae,
walifurahi
sana maana siku hiyo walikurupushwa na mgambo wa jiji,
wakapoteza makopo yao waliyokuwa wakipeleka
kuuza kiwandan,
istoshe walikuwa na njaa kubwa sana
Yoshua
alikuwa ameajiriwa kwenye duka moja kubwa
la
tajiri moja mkubwa ambaye alikuwa ni naibu waziri hapa nchin
Yoshua
akawapa chakula pia wakatafuta mahali pa kupata maji ya kuoga
maana siku ya tano hawajaonana na maji kutokana
mahangaiko yao.
Walimwelezea
rafiki yao huyo shida wanazopata
kutokana
na kurupushan za jijin,hivyo hawana kibarua
basi
rafiki yao aliamua kuwapa kibarua cha kutembeza bidhaa
za
pale dukan ili angalau awe anawapa chakula na sehem ya kujihifadhi
SAFARI
YA MAISHA YAO
katika
kijiji hiki wanatokea vijana wawili wanaopendana sana
kijana
wa kwanza anitwa mussa na wa pili haruna
haruna
alibahatika kupata elimu mpaka kidato cha sita mussa yeye alikuwa kijana wa
mtaani alishindwa kwenda shule kutokana na matatizo ya kifedha,
waliishi
kwa furaha sana huku wakisaidiana kwa namna moja ama nyingine.
waliishi kwa muda mrefu sana kijijin pale kwa
bahati mbaya haruna alishindwa kuendelea na elimu ya chuo kikuu baada ya kukosa
mkopo wa serikali
aliamua
kujiunga na mussa kufanya vibarua pale kijijin
mussa
alikuwa akiishi na mama yao tu ,baba yao alikufa akiwa na miaka kumi pekee. Mwaka
mmoja baadae mama yao mzazi aliigua kwa muda refu
lakin
kutokana na umasikin mama yao alijitahid kufanya kazi ngumu inagawa bado
alikuwa mgonjwa. Kutokana na hali ile mama yake alifarik baada ya
kuugua
maradhi ya kifua kutokana na kufanya kazi ngumu
wadogo
zake mussa wengine waliacha shule na kuanza
kuufanya
kazi ya kuuza karanga na pipi
baada
ya mussa kuachiwa majukumu ya familia aliamua
kumwachia mdogo wake familia ili aende mjini kuwatafutia wadogo zake chakula na
ada ya shule kwa wadogo zake wawili
wa
kike waliokuwa bado wanasoma shule ya msingi
familia
yao ilikuwa ya watoto watano yeye akiwa wa sita, hakuwa na uchaguzi
hivyo
basi ilimbid akimbilie mjin kutafuta maisha
aliongozana
na haruna ambaye alitoroka kwao,
wakalekea
jijin dar kwa usafiri wa tren, mwisho walifikia dar lakin wasijue pa kuelekea
JIJIN
DAR
baada
ya Yoshua kuwapa hifadhi hiyo ,basi ilibid warudi kwa marafiki zao
ambao
waliwapokea siku ya kwanza kufika dar maeneo ya gongo la mboto
ambako
ndiko walifikia kwa mara ya kwanza kabisa.
Njian walikutana na majirani wakiwa wamejaa
maeneo hayo
jamaa
mmoja akawavuta pemben kwa ghafla akawaambiwa
“wenzenu wale wameshikwa na police, na nyie
mnatafutwa, wamekamatwa na kesi ya kuuza bangi na wizi, na wanashutumiwa kesi
ya ubakaji
mussa
na haruni ilibidi wakimbie na kwenda mpaka tabata MAWENZ
walipofika
basi walinyamaza bila kumwambia Yoshua
kesho
yake wakaanza kibarua chao huku wakijihadhari sana na ule mkasa uliotoKea jana
yake. Maisha yaliendelea na kibarua chao kilwapatia mkate
mussa alikuwa akiikumbuka familia yake kwa
kidogo kile familia aliyoicha nyumban,
ndugu
zake wengi walianza kushtumu kitendo kile cha mussa
kutelekeza
famailia yao kwa kuiacha familia katika mazingira magumu.
aliishi
kwa miaka kama miaka 3 bila kurud kwao, lakin kwa kias Fulani aliweza
kuwasaidia wadogo zake sana kwa kila alichopata
AKUTANA
NA MAURINE
maurine
alikuwa mwenye furaha sana kila walipokuwa wakikutana.
Kila
jion baada Ya kazi walikuwa wakielekea kwenye mgahawa mmoja karibu
na
nyumba aliyokuwa akiishi maurine, maurine aliipenda sana kampan yake,
alitokea
kumwamini sana mussa, alimweleza kila kitu kuhusu maisha yake ya nyuma.
maurine
alimwambia kuwa yeye anapenda sana kusoma
lakini
hawezi kuendelea na masomo tena kutokana na maisha
maurine
alimwambia kuwa wazazi wake walikuwa matajiri wakubwa sana
waliishi
dar, lakini yeye aliishi morgoro kwa bibi yake. Akamwelza….
“siku
moja ndugu yake mdogo baba aliyekuwa anaishi morogoro alikuwa akifunga harusi.
Siku
hiyo Baba, mama na wadogo zangu walikuwa wakitokea dar na gari yake kuja
morogoro Kwenye harusi ya mdogo wake, mimi nilimwaga bibi Nikaelekea stand kuu
moro
ili kumpokea baba. nilienda stand saa 6 mchana
kuwasubiria
muda mrefu ulipita bila kuwaona baba na mama
na wadogo zangu watatu,
nililia
sana kwanini baba na mama walinidanganya, niliamua kurudi nyumban.
Niliamua
hata nilisusa hata kwenda harusini yay a baba mdogo.
nilipofika
nyumban bibi aliniambia labda wamepata dharura nilimkuta bibi anangalia tv,
baada
ya dakika kadhaa walikuja watu watatu nyumban, wakamwomba sana bibi
aende
hospitali ya mkoa. Tulipofika hospitalin tulimkuta baba mdogo
amelazwa akiwa na suti yake tulishangaa na
kupigwa na butwaa,
hakuna
aliyejua kwanin amelazwa watu walikuwa na huzun wegine walikuwa wanalia tu
ghalfa
shangaz nae aliletwa akiwa amepoteza fahamu
bibi
alishindwa kuvumilia akawa anapiga makelele akitaka kujua kwanini mwanae
kitinda mimba amelazwa maana hakuna aliyemwambia baba mdogo kafanyeje.
mkewe
alikuwa pemben na shela asijue cha kufanya nilitoka nje kumtafuta baba na mama
nikiamin kuwa walikuja hospitalin ndio maana hawakuja stand,
nilihangaika
hospital nzima lakin cha ajabu sikuweza kumwona yoyote
niliwalaum
sana wazaz wangu kwanini ndugu yao kalazwa hawajaja
baba
alikuwa mlevi sana, niliamin atakuwa amepita bar na asijue kinachoendelea
baada
ya muda baba mkubwa alikuja macho yakiwa mekundu,
akawa
analazimisha turud nyumban lakini nilikataa katakat,
nilimuuliza
baba mkubwa kuwa baba yupo wapi akaniambia baba yupo nyumban,
sikumwaga
mtu yoyote niliondoka kwa spidi nusura nigongwe na pikipiki
ili
nimuwah baba na mama niwape taarifa nilipofika nyumban sikuwona mtu yoyote
nilipoingia
ndani nilikuta tv aliyokuwa anaangalia bibi bado inawaka
wala
hakukumbuka kuizima wakati ule alipopea taarif aende hospital,
lakini kwenye tv ilikuwa inaonesha taarifa ya
habari, lakin cha ajabu
nilishangaa
kuona taarifa ya kusikitisha sana, nikiwa naendelea kuangalia sikuweza kuamin
nilichona, msomaji wa habari alikuwa akisoma taarifa moja ya kusikitisha sana,
ilikuwa
ni taarifa hyo iliyohusu familia moja iliyokuwa ikitokea dar kwenda morogoro
imepata
ajali baada ya kugongana na semi iliyoshindwa kukata kona na kuivaa gari ndogo
na watu kwenye gari hiyo ndogo wamefariki dunia pale pale.
Lakini
majina yao hayakuweza kupatikana mara moja kwa sababu
miili ya marehemu iliharibika n haikuweza
kutambulika mara moja.
Nilihisi
kama naangalia filamu, sikutaka kuamini kama ni familia yetu,
Nilijkuta
napiga mayowe bila kujitambua, nikaona haitoshi
basi
nikatoka spidi nyumban kurud tena hospital, nilipofika hospital
nilikuta bib nae kalazwa, nikajua basi tayari nimebak
peke yangu
nilihisi
dunia yote imeniangukia. sikuwa na cha kufanya, nililia mpaka nikazirai.
MAISHA
YA MUSSA
maisha
ya musa yaliendelea huku akifurahia kibarua chake maana kiliweza kumpa kidogo
kitu
alikutana
na dada mmoja aliyekuwa akiiuza duka ambalo alikuwa akipeleka oda
waliishia
kuwa marafiki hasa kutokana na utan wao
kila
siku walipokuwa wakikutana basi walitaniana sana
dada
huyo alikuwa mzuri sana wa sura, dada huyo alimpenda sana mussa
jion
baada ya kaz dada huyo alikuwa akimpitia mussa kuelekea nyumban
siku
nyingine walienda kwenye vibanda vya video au hata wakati mwingine
walienda
nyumban kwa dada hyo na walipika wakala
wakati
wa usiku musaa anarudi kwenye kibanda chake alichopangisha na haruna
mussa
alikuwa mcheshi sana ndio maana dada huyo alimpenda sana
mussa
alimficha sana kuhusiaana na maisha yake
lakin
haruna aliamua siku moja kumweleza yule dada historia yao
haruna
alimweleleza namna maisha ya mussa ya zaman yalivyokuwa
dada
yule aliumia sana moyo kutokaana na ugumu wa maisha yake mussa
jonhson
nae alikuwa alikumsumbua sana dada yule kila siku hasa akienda dukan pale
alikuwa
akimnyanysa na mshahara wake, na pia wakati mwingine
baada
ya kumweke mshahara wake benki alimwita nyumban ili tu ampe mshahara wake
jonson
alikuwa mtoto wa bossi hivyo maurine hakuwa na uhuru,
jonson
alimtaka sana huyu mdada kwa nguv zote lakin mdada yule hakumpenda hata kidogo
siku
moja jonson alimwona mussa akiwa na maurine
alikasirika
sana , na alikerwa sana na kitendo kile
na alitaman sana hata amfukuzishe kazi mussa kwa sababu Yoshua nae aliajiriwa
na Jonson. Hivyo Jonson alikuwa na uwezo
wa
kumfukuzisha kazi maana kampuni ile ilikuwa mali yao
TUNAENDELEA
mussa
alikuwa akipokea sana pesa kwenye mpesa yake na asijue ni nan anaemtumia
lakin
kwa kuwa alikuwana na maisha magumu aliamua kutuma pesa zile nyumban
hata
wadogo zake walioacha shule walianza kwenda tena shule
alitaman
sana kurud nyumban lakin aliona aibu barua zilikuwa zikija kutoka nyumbna kwao
Hatimaye
wadogo zake waliamua kuhamia kwa bibi yao
Lakin
huku mjini urafiki wa mussa na maurine ulizid sana
na
kitendo kile kinaonesha kilizid kumuumiza sana jonson kichwa
na
aliamua kumtumia meseji za matus mussa na vitisho kwa maurine lakin maurine
hakujali hilo,
siku
moja jonson alituma watu kumkamata mussa kwa nguvu
Na kumchukua kwa nguvu mpaka nje ya mjin, kwa
bahati nzuri maurine na haruna waliona tukio lile hivyo taaratibu waliamua
kufuata nyuma
na
walipofika maeneo hayo, kwa bahat mbaya jonson aliwaona
kuwatuma wale vijana wawakamate wote wakaletwa
eneo walilokuwa
wakati
wanaongea hayo haruna alikuwa akirecod sauti kwenye simu yake
kijana
mmoja alimshtukia haruna,akamsearch akamkuta na simu ikiwa inarecord,
jonson
kwa hasira alichukua simu ile na kuipasua yote, akawaagiza vijana wale
wawakague kila mmoja mfukon mwao, kumbe maurine nae alikuwa akirecord tukio
lile kwenye simu yake
jonson
akaichukua simu ile alipotaka kuivunja, maurine alimwomba akampigia magoti
akamwambia
chukua memory card pasua ila naomba unipe simu yang ina oda za kazin na mambo
muhimu ya kazini, kwa kuwa jonson anampenda sana maurine na hizo oda ni za duka
lao, alitoa memory akaificha na kumrudishia simu yake, baadae waliwaachia na
wakurudi zao nyumban
mussa
alitaka kuachana na msichana yule maana alikuwa akimwingiza
kwenye
matatizo mengine, maurine alikataa kata kata, haruna alimshauri sana mussa
aachane nae
MAURINE
AZINDUKA
Baada
ya kuzinduka niliwakuta ndugu zangu wengi Wakiwa pemben yangu wakinipa pole
Sikutaka
kuamin kilichotokea Nilitaman sana habari ile siyo ya familia yetu
Ilibid
watu watangaze kuwa harus ile imeahrishwa, Maana watu walikuwa wakisubiri
ukumbn
Inasemekaa
kwamba Waliokuwa kanisan walisema kuwa, baada tu ya harusi kufungwa
Waleiekea
kwenye hotel moja kwa ajil ya picha
Wengine
walisema Kabla ya tukio hilo la harusi inasemekana kwamba
Shangaz
alikuwa akiwasilina na kaka yake ambaye ndiye baba yangu,
Shangazi
aliona kimya kwa muda mrefu na wakati mwingine meseji zilikuwa haijibiwi
Akaamua
kumpgia simu kujua wamefika wapi mbona wamechelewa
Ghafla
alipokea mtu mwingine ambaye alijtambulisha kwa jina la traffic james,
akimweleza kuwa wanaempigia simu hayupo tena
dunian na
wote waliokuwa kwenye gari hiyo wamepata ajali
na wamefriki wote
Shangaz
alimkimbilia baba mdogo na kumweleza alichoambiwa, baba mdogo alizirai pale
pale.
********************************************************************************
ilipofika
kesho yake baada ya tukio, mapadre walifika hospitalin
Kumwangalia
baba mdogo lakin bado alikuwa hajazinduka
Tulirudi
nyumban, watu wakaja nyumban wakawa wanatupa moyo
Baba
mkubwa alikuwa akisema millin ya marehe haiwez kuagwa kwa kuwa iliharibika sana
Madaktar
wakasema kuwa ni mtu mmoja tu ndiye mwili ulibak \wengine wote walisagwa na
gari, sikutaka kuamin maneno ya madaktari
Nilitaka
niwaone hivo hvo ila walinizuia kabisa nisiangalie miile ile
umati mkubwa hasa wale waliokuwana kadi za
harusi wote ulikuja kuzika familia yetu
Baba,
mama, wadogo zangu watatu, junia aliyekuwa darasa la 3, Erick aliyekuwa darasa
la 5 na Helen aliyekuwa form one
Ulikuwa
ni mzigo ambao nilishindwa nifanye, Na wakati ule nilikuwa najiandaa na mtihan
wangu kidato cha nne Nilichanganyikiwa kabisa
tuliwazika
salama lakin baba mdogo hakuzinduka bado, nilifanya mtihan ule kwa tabu sana
Baadae
baba mdogo alizinduka lakin alichanganyikiwa kabisa
Mpaka
leo baba mdogo ana matatizo ya akili na amekuwa akianguka ghafla mara kwa mara
Matokeo
ya form 4 yalitoka cha ajabu mbali na hali nilifaulu
Mama
mkubwa ambaye alikuwa mke wa kwanza wa baba
Alikuja
na kutaka mali za baba kwa kigezo kwamba alichangia mafanikio yale
Hivyo
anapaswa apewe jukumu la kunilea na kunisomesha maana baba mdogo alikuwa
mgonjwa
Mama
mkubwa Yule alikuwa mwansheria, alipoenda mahakaman alishinda kesi ile hakuna
aliyejitetea, alinichukua nikaish dar na Nilishi nae pamoja na mume wake, lakin
mama mkubwa alikuwa akintesa sana. Wakati ule nilikuwa kidato cha tano
Nilisoma
kwa tabu, alinipelekesha sana, nilivumilia sana lakin nilishindwa
Nikamaamua
kuodoka nyumban na kuanza kujitegemea
Nilimwibia
zaid ya million 5 nikakimbia nyumban
Polis
walinitafuta na aliniweka rumande kwa wiki moja bila kutoa taarifa kwa ndugu
zangu wengine morogoro,
Nilipulizwa
kuhusu hizo fedha nilikataa kabisa kuwa sikuchukua pesa ile
Baba
mkubwa alipopata taarifa alikuja akanitoa rumande
Niliisha
kwa baba mkubwa, baadae alinitafutia kazi kwa rafiki yake ambaye ndiye baba
yake jonson, baadae baba mkubwa alihamishwa kikazi mbeya
Akaamua
kunitafutia chumba cha kuish ambapo ndicho hiki unacho kiona
Niliahamishia
maisha yangu hapa, nilichukua ile million 5 nikajisomesha baadhi ya course za
sheria, nikfanya mtihan wa kidato cha sita lakin sikupata matokeo mazuri sana,
nikawa
najisomesha open university, Hayo ndiyo maisha yang kaka mussa
*********************************
Siku
moja jonson alienda dukan alipokuwa anauza mauirine, maurine alikuwa anajisikia
homa siku hyo, akapitiwa na usingizi, akaamua kulala kwenye meza hapo dukan,
Jonson
akaingia ndan, akakuta simu yaya maurin ipo mezan, Akachukua simu ile
akaangalia baadh ya meseji
Mara
ikaingia mesesj ya mpesa alipoifungua akakuta kuwa
Maurine
kuna namba ametuma mpesa laki moja
Jonson
alipoangalia aliyetumiwa akakutana na jina
la Mussa Jango
Jonson
akafunga simu ile akarudisha mezani Akaondoka kwa hasira bila kumwamsha maurine
Akamfuata
rafiki yake aitwaye festo,akamwelezea kwamba maurine
Anamtumiaga
pesa mussa, festo akamshauri arudi tena pale dukan
Akimkuta
bado kalala basi achukue pesa iliyopo kwenye droo.
Jonson
akafanya hivyo, ikawa kila siku akienda dukan anachukua kiasi chochote cha pesa
Baadae
basi jonson alikuja ili afunge mahesabu, ikaonekana hasara kubwa sana
Jonson akataka kumfukuza kazi, baba yake jonson
akapewa taarifa
Jonson
akamweleza baba yake kuwa pesa zimepotea, festo akashauri kwamba
Waende
voda shop kubwa waangalie kama huyu dada anatumga pesa kisiri
Walipoongalia
walikuta anamtumia pessa Mussa Jango
Baba
yake jonson akaomba huyo mussa atafutwe mara moja
******************************************
ITAENDELEA, HII NI RASIMU YA KWANZA, KAMA UNA USHAURI, MTAZAMO AU CHOCHOTE NJOO KWENYE 0763370020/ 0713960030 privashayo@gmail.com facebook Priva abiud
ITAENDELEA, HII NI RASIMU YA KWANZA, KAMA UNA USHAURI, MTAZAMO AU CHOCHOTE NJOO KWENYE 0763370020/ 0713960030 privashayo@gmail.com facebook Priva abiud

Leave a Comment