DE GEA ABAKI UNITED, MADRID KUISHTAKI UNITED, MARTIAL ATUA UNITED, DE BRUYNE SASA RASMI,,,,,,?

 

Na Priva Abiud


Hizi ni habari zilizogonga Vichwa vya Habari


HAYAWI HAYAWI..SASA YAMEKUA.. KILE KILIO CHA WANA MAN UNITED KUTAKA DAVID DE GEA KUBAKI UNITED BASI CHATIMIA. 

Taarifa kutoka kwa Mwandishi wa Sky Sports jijini madrid zinasema kuwa, Van Gaal na Jopo lake wamefanya uharamia kama ule wa Coentrao kujiunga na Man United. Baada ya timu zote kukubaliana, mpaka kufikia saa tano kamili usiku Manchester united hawakupeleka data, wala kumbukumbu zozote ili kukamilisha usajili huo wa milioni 29 pamoja na Kelyor Navas. Inasemekana kuwa huenda Madrid wakaishtaki Man united Fifa kwa uhuni ule. Hivyo De Gea hayupo kwenye listi ya kikosi cha Madrid kilichosajiliwa La Liga Msimu huu. Ligi kuu ya Hispania imefunga usajili wake lakini bado EPL mpaka leo saa sita usiku. Inasemekana Baada ya kumbukumbu kucheleweshwa Madrid walipandisha Dau lao mpaka kufikia Million 45 lakini bado hakuna Majibu yoyote yaliyopatikana kwa wakati ule. United wamekanusha kwamba walipeleka nyaraka za usajili baada ya dirisha kufungwa na wamesema hayo ni masuala ya kibiashara ya ndani ya timu. Man united huenda wangepata faida ya million 11 katika usajili wake kwani walimsajili kwa ada ya milion 18 mnamo mwaka 2011 na wamedai wapo tayari kumpoteza bure. Wanaiman kuwa atavunja record ya golikipa wa Italia Gianluigi Buffon aliyesajiliwa Million 32 akitokea Mparma 2001. Sasa itabidi mke wake Ambaye. Ni mcheza Pop Bi Edurne Garcia kurudisha kiherehere Chake bbaada ya kutafuta nyumba madrid


Source Sky News

Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Mexico Javier Hernandez (chicharito) amejiunga na Bayern Iiverkusen kwa Ada ya Paundi million 9, na amesaini mkataba wa Miaka 3 na kukabidhiwa jezi namba 7, chicharito alijiunga na man utd mwaka 2010 na kufunga magoli 59 kwenye michezo 152 aliyoichezea Man Utd,

huku Adnan Januzaj Akijiunga na Borussia Dotmund kwa mkopo wa Muda mrefu. Hapo hapo mshambuliaji wa Monaco Anthony Martial Amejiunga United kwa Ada ya Paund 36. Mshambuliaji huyo aliyefunga magoli 9 kwenye michezo 35 msimu uliopita ambaye ana Miaka 19 ameshafanya vipimo vya afya hivyo muda wowote atatambulishwa Rasmi na Man Utd... Source Sky Sports

Kelvi De Bruyne amekabidhiwa Jezi no 17 pale the Citizen. Amekamilisha usajili wa Paund 56 akitokea Wolfburgs na kujiunga na Man city.

Ndugu zangu wa Anfield wao wamempata kinda Owonyi mwenye miaka 18. Taiwo amejiunga na liverpool akitokea Frankfurt kwa mkopo.

Mourinho amefanya usajili wa Beki kutoka Nantes Papy Djilobodji na ameshakamilisha vipimo vya afya.

Hata hivyo kule Hispania
Raul Garcia amekubaliwa ombi lake la kutoka atletico na kujiunga Athletic Bilbao, hivyo rasmi sio mchezaji wa Madrid tena. Amesaini na wanabasque miaka 4.

Villareal imemnasa mshambuliaji wa Porto Adrian Lopez kwa mkopo

Kule Ujeruman sasa

Draxler ameondoka Schakle 04 na kujiunga Wolfsburg. Baada ya De Bryne kuondoka huyu amekuwa Mrithi wake! Draxler alijiunga klabun hapo akiwa na miaka 17 na alicheza michezo 119 na kufunga magoli 18.

Tutazidi kuhabarishana endelea kutufuatilia zaid.

No comments

Powered by Blogger.