SAKATA LA PEDRO LILIVYOKUWA
Na Priva Abiud
 |
| PEDRO RODRIGUEZ AKIBUSU KOMBE LA UEFA SUPER CUP |
|
|
wakati pedro akipanda ndege kuelekea london magharibi, ukweli ni kwamba aliyefanya usajili huu ukakamilika ni swahiba yake mkubwa cesc fabregas kumpa Jose Mourinho namba ya simu ya pedro kisha kumpigia Pedro na kumweleza kuwa hatma ya maisha yake ipo london sio manchester hivyo asipoteza muda wake, mpenzi wake Pedro Danila Semann pamoja na mke wake Carolina Martin walifanya kazi ziada katika kumshauri Pedro. taarifa zinasema kwamba hata hivyo CEO wa Man utd bwa Ed Woodward alipanda ndege kuelekea jijin barcelona na juzi jumatano alidai kuwa kila kitu kilikuwa sawa, lakin nyuma ya pazia ukweli ni kwamba mtendaji wa chelsea bwana Marina Granoskaia alikuwa na mazungumzo ya siri baina yake na pedro pamoja na wakurugenzi wa barcelona ndio maana hata usajili huu ulikuwa unakwamakwama hata pale kocha mkuu wa barcelona aliposhindwa kutolea maelezo suala lile.
 |
| PEDRO AKIWA FABREGAS |
|
inasemekana kwamba Pedro amesikiliza zaid ushauri wa Hristo Stoichkov kuwa asikubali kujiunga na Louis Van Gaal kuwa ni mharibifu na asiye na malengo mema na Man utd maana anaenda kuiharibu Man utd muda sio mrefu. hata hivyo Hristo alitumia muda mwingi kuwashauri fabregas na Mourinho wafanye mpango wa kumnusuru kijana yule. Hristo anamtuhumu Van Gaal kipindi anafanya nae kazi Barcelona kuwa alitaka kuua kipaji cha Romario na rivaldo istoshe hata pale alipokuwa Ajax Amsterdam alipuuza kiwango cha zlatan ibrahimovic mbali na hilo hivi majuzi ameonekana kumnyanyapaa kipa wa kihispania Victr Valdes.
Leave a Comment