MICHUANO YA MBATIA CUP YAFIKA PATAMU

Na Mwandishi CALVIN mtenga Moshi

Njia Panda Fc 1~4 Agip Fc
Himo United 2~1 Chekereni Fc
Michuano ya Mbatia cup katika jimbo la Vunjo
Mkoani akilimanjaro imeendelea kushika kasi tena
ambapo imeingia katika hatua ya robo fainali na
kushuhudia Timu kubwa kadhaa zikitoana jasho
patashika nguo kuchanika ambapo tulishuhudia
michezo miwili ikifukua nyasi katika kiwanja cha
njiapanda himo ambapo mchezo wa kwanza
ulizikutanisha timu za Himo United dhidi ya
Chekereni Fc na katika pambano la pili
tulishuhudia mechi kali na yenye ulinzani mkali
kati ya wenyeji Njiapanda Fc dhidi ya timu makini
sana kutoka Kahe Agip Fc.
Katika mechi ya kwanza iliyoanza kutimua vumbi
kwenye majira ya saa nane mchana tulishuhudia
mechi kali na yenye uhondo wa hali ya juu kati ya
Chekereni Fc dhidi ya Himo united ambapo timu
ya Himo ilichomoza na ushindi wa goli mbili kwa
moja kutoka kwa Chekereni Fc ambapo timu ya
Chekereni ndiyo iliyoanza kujipatia goli la
mapema kabisa katika kipindi cha kwanza kupitia
kwa mshambuliaji wao aitwaye Ndella na goli hilo
lilidumu hadi mapumziko lakini mambo
yalibadilika gafla katika dakika za mwanzo za
kipindi cha pili kwa timu ya Himo United kujipatia
mabao mawili ya haraka ndani ya dakika tano
kupitia kawa wachezaji wake hatari kabisa
Maradona na Pacho ambapo inaonekana magoli
hayo yametokana kutokana na uzembe
uliofanywa na walinzi wa timu ya Chekereni na
kufanya timu ya himo kujinyakulia ushindi na
kukata tiketi ya kucheza karika hatua ya nusu
fainali ya michuano hiyo ymiliyadhaminiwa na
ndugu James Mbatia na kupewa jina la Mbatia
Cup...
AGIP FC 4~1 NJIAPANDA FC
Lakini pia tulishuhudia pambano lingine la kukata
na shoka kati ya wakali Njiapanda Fc dhidi ya
timu yenye washabiki wengi kutoka Kahe iitwayo
Agip Fc ambapo mechi hiyo ilimalizika kwa
Njiapanda Fc kulala kwa idadia kubwa kabisa ya
magoli 4~1 huku timu ya Agip ikionekana
kutawala vyema mchezo kwa kucheza soka zuri
na la kuvutiavna kuwaacha wachezaji wa
Njiapanda Fc wakihaha wasijue la kufanya. Mechi
hii ilichezwa kwenye mishale ya saa kumi ya jioni
katika kiwanja chenye kiwango cha TFF kiwanja
cha Njiapanda na hivyo kumaliza kabisa
matumaini ya Timu ya njiapanda kufuzu kwa
hatua ya nusu fainali. Magoli ya Agip yalifungwa
na Ally Bakari, Aume Temba, Beny na Waliii huku
goli la Njiapanda Fc likifungwa na mshambuliaji
Rama na hivyo kuwa kama kifuta machozi kwa
timu hiyo ya Njia panda. Pia katika pambano hili
tulishuhidia ugomvi kadhaa kati ya mashabiki
wenyewe uliosababishwa na imani za kishirikina
na kufikia hatua hadi ya washabiki kutaka
kupigana.
Michuano hii itaendelea tena katika hatua ya
nusu fainali itakayopigwa hapo siku ya ijumaa
kwa kuzishuhudia timu zilizofuzu zikicheza ili
kusaka nafasi ya kucheza katika hatua ya fainali
ili kuweza kuzitwaa hizo shilling millioni mbili
kama zawadi ya mshindi wa kwanza wa
michuano hii.
Bila kusahau mashindano haya yamedhaminiwa
na mgombea ubunge jimbo la Vunjo ndugu James
Mbatia kupitia chama cha NCCR MAGEUZI 2015..

No comments

Powered by Blogger.