NANI KUSHUKA DARAJA? ARSENAL JE??
KIJIWE CHETU
NANI ATASHUKA DARAJA? ARSENAL JE?
Roma Mkatoliki alisema hivi "bandugu Bwaga manyanga, ayaokote magufuli" pia akasema hivi "najua mvi sio busara ila naomba aman itawale" kweli manyanga yalibwagwa magufuli akayaokota, ila tatizo wanagombania ikulu, lugha za kampeni zao kuwapa kipato wananchi kisa anauchukia ufisadi. Yetu macho je Lowasa atabeba kombe? arsenal? Je magufuli atashusha madaraja?? October
****************************************
Twende kazi....................
Wakati kichwa changu kikizungukwa na maswali mengi ya kisiasa kutoka kwa watu mbalimbali, binafsi nmekuwa na maoni yangu moyon. Kwanza nianze na la kushuka daraja! Msimu huu kuna timu ambazo sioni maisha yao EpL tena, kama vile sunderland, watford na Norwich city! Kwa klabu zilizopanda daraja kiasi fulani nawasuport hawa Bournemouth! Unaweza kujiuliza ni kwanini. Nmejaribu kuwafuatilia hawa jamaa kujua siri ya mafanikio yao! Kwanza mmiliki wa klabu hii Mrusi Max Demin, amefanya usajili wa pesa kubwa sana, kama Tyron Mings paund 8 kutoka Epswich, Max Gradel paund 7 kutoka st Etiene na Paund 3 kwa Tomlin Wa middles!Hakuna klabu ndogo imefanya hivi.
***************************************
PILI.........
Kocha wake mkuu bwana Eddie Howe kwanza anajiamin, na anajua anachokifanya! Alisema kuwa, hahitaji mchezaji mkubwa ambaye atajaza nzi kwenye vyumba vya kuvalia nguo, anataka wachezaji wenye uwezo sawa! Amempata mchezaji wa zaman wa united Josh King, pia christian atsu wa chelsea, ameshasajili wachezaji 9 mpaka sasa! Sunderland naona wanawapoteza kabisa coates, kaboul, jeremiah lens na Adam Mathew sidhan kama kocha Dick Advacaat atawabakisha!
*************************************
NIRUDI MPAKA LONDON
ningependa nikae na Wenger nmpe moyo kidogo! Mimi sio mshabiki wa arsenal, lakin kwa msimu huu napiga kura yangu kwao (chadema) wamekaa muda bila kwenda ikulu, wanadhiki ya muda mrefu, wamejipanga sana wametukanwa vya kutosha.
*********************************
Arsen Wenger amepitia kipindi kigumu cha kukosa pesa kutokana na Madeni, kwa namna navyowaona watafanya vizuri, Giroud atapata magoli Mengi, ila Pal Mertesucker apigwe chini achezeshwe Gabriel Paulister. Tena Kwa sasa wamepata kipa Mzoefu na Mwenye uwezo na mbinu nyingi. Ikumbukwe kwa sasa huyu ndiye kipa mwenye record bora zaid kwa pale England na hata ulaya.
****************************************
Nataman sana maana huyu mzee ameteseka sana, atleast afike nusu fainal Uefa, abebe tena Fa au ligi kuu, achukue ubingwa wowote mkubwa kama watapata nafasi hiyo! Siwapi nafasi united Van gaal ni kichwa cha Mwendawazimu amekurupuka kusajili wachezaji wengi huku akisahau anatatizo la beki wa kati na kipa ambaye De Gea hati hati, Mourinho hana mbinu tena, liverpool asanteni kwa kushiriki. Hata kama wewe ni mwanaunited basi hebu tuweke roho mbaya pembeni mwenzenu hajui utamu wa ikulu******************
PIA KAMA KIJANA MWENZANGU, POPOTE ULIPO KAJIANDIKISHE KUPIGA KURA! USIKOSE NAFASI HII YA KIPEKEE KABISA! TUPATE MABADILIKO! TUMIA HAKI YAKO VIZURI.
Leave a Comment