VAN GAAL AKUMMBWA NA MKASA MWINGINE, MOURINHO AJIGAMBA


VAN GAAL AKUMBWA NA MKASA MWINGINE, MOURINHO AJIGAMBA
 Na Priva Abiud

Ikiwa ni katika harakati za kujenga kikosi chake kwa ajili ya msimu huu ambao tayari umeshaanza, kocha wa manchester united loius van Gaal amekumbwa na kikwazo kingine cha kumsajili Sadio Mane wa Southampton. kocha mkuu wa Southampton Ronald Koeman amesema hakuna mchezaji yoyote anauzwa, Huu utakuwa mkasa mwingine kwake gaal ikiwa atamkosa mane baada ya otamend kujiunga man city huku De gea hali yake ikiwa njia panda baada ya Jorge Mendes kuonekana jijin manchester mara baada tu ya kufunga harusi yake wala hajaenda kula fungate bali alifunga safari mpaka london na hatimaye manchester ili kukutana na mteja wake. ikumbukwe kuwa Koeman hawana mahusiano mazuri na Van Gaal. katika mkutano wa waandishi wa habari AVG amesema kwamba taarifa za kununuliwa kwa Pedro zilisambaa sana magazetini, hivyo hakuwa na shida nae "kama ningemtaka Pedro ningemchukua, wala msimlaumu sana Ed Woodward kwa sababu sikumuagiza kumnunua Pedro, waandishi wa habari wanaweza kuandika chochote tunachokitaka lakin hawawezi kutuambia wanachokitaka" hayo ni maneno ya AVG akimaanisha kuwa magazeti ndio yalizusha na kusambaza habari za Pedro kuliko ukweli uliokuwepo hapo awali.
 United boss Van Gaal will address the press amid more Bale speculation
hata hivyo van gaal amesema mchezaji anaemhitaji kwa sasa ni Gareth Bale wa Real Madrid maana anaamini kuwa yeye ndiye anayeendana na  mfumo wake wanoutaka pale carringhton.

pia Mourinho amejibu hoja za wengi waliokuwa wakiuliza juu ya fitina na hujuma alizofanya juu ya man utd, alijibu akasema, "pedro ameonesha moyo wa kweli na sisi, maana anatamani kucheza, kushinda mataji na kuwa na furaha, siwezi kusema kuwa sisi tumeshinda man utd wamepoteza hapana...huu ni muda wa Pedro kushangilia na kufurahia sio sisi" ukijaribu kuangalia kauli za makocha wote wawili utagundua kuna sizitaki mbichi hizi pia kuna kauli ya sio mimi ni yeye.
  hata hivyo kuhusiana na suala la mane ni kwamba mashabiki wengi wa southampton wamesikika wakisema Mane Dont  Go" hili limezua hisia mpya pale mane alipoonekana akiwabusu watoto wadogo waliokuwa mashabiki wa klabu hiyo, hali ya hewa inaonekana kuwa mane hatoondoka klabuni hapo. manchester united imepeleka ofa ya kushtukiza ya paund 15 kwa ajili ya kumnasa kinda huyo aneyechezea pembeni mwenye miaka 23 lakin inaonekana kugonga mwamba.Manchester United target Sadio Mane has declared his intention to stay at Southampton

No comments

Powered by Blogger.