VAN GAAL ASHAMBULIWA TENA

Mchezaji wa zamani wa Man United, Garry Neville ameiambia sky sports kuwa Van Gaal anapswa kumpa Wayne Rooney Uhuru wa kucheza. Alisema kuwa "Van Gaal anahitajika kumpatia Rooney uhuru zaidi wa kucheza namba sahihi kuliko jukumu alilo nalo kwa sasa"

Mbali na wayne Rooney kufunga Magoli matatu katika mchezo wa Uefa dhidi ya Club Brugge Wayne Rooney ameshindwa kufunga goli lolote kwa takriban masaa 14 na dakika 24. Rooney amecheza kama namba 9 katika michezo yote, van gaal amemchezesha katikati ya mabeki wawili wa katikati ambao wanampa tabu sana Rooney kufanya vizuri.

Hiyo sio nafasi ambayo Rooney amecheza kwa takribani miaka 11. Hii ndio sababu kubwa ambayo inamfanya Ander Herrera asicheze sehemu ya kiungo kwa sababu anapitiliza majukumu yake! Van Gaal anapenda zaidi wachezaji kucheza katika nafasi zao na sio vingenevyo.

Carragher pia ametia chumvi baada ya kulaumu sana katika mchezo wa swansea ambapo anasema, Rooney hakuonekana kimchezo, na kumtoa nje ilikuwa ni Riski kubwa zaidi kuliko kumpa jukumu lingine uwanjan.:)

No comments

Powered by Blogger.