ACHENI UPOTOSHAJI DHIDI YA UISLAM

New York. Na Priva Abiud

Waislaimu kote duniani wameendelea kulaani mauaji ya Waislamu wenzao Duniani, huku wakiishtumu Marekani na nchi nyingine ambazo zinachukulia Uislamu kama dini ya kigaidi. Viongozi wa kiislamu wamelaumu sana Mauaji ya Kikundi Cha ISIS ambacho wanaua waislamu wasiokuwa na hatia.
"""""""""""""""""""

Kiongozi mmoja alisema kuwa, "inawezekanaje kikundi kidogo cha watu kikawakilisha Uislamu kote dunian? Na je kama ni kikundi cha kigaidi dhidi ya Wasio waislamu inakuwaje kimeua zaidi ya Nusu ya Waislam hapo mashariki ya kati?"
*******************************

Kiongozi huyo ambaye hakutaka Jina lake litajwe alisema, waathirika wakubwa wa Ugaidi ni waislamu, akaongeza, "asilimia 90 ya mauaji haya yanatokea Nchi za Asia, ambako walio wengi ni waislamu, wengi wao wamepoteza Maisha na Familia, sisi hatuchangamani na kikundi hiki kinachotuua sisi waislamu wenzao, pia wakristu wanateseka, na hata Yazidis" "kama kweli kikundi hiki ni chema kwetu sisi Waislamu mbona walimuua Proffesor wa kiiraq aliyekuwa muislam mwenzetu"
*******************************


Kwa mfano pia kule Marekane, Bomu lilipigwa pale Boston kwenye mashindano mwaka 2003, waislamu Na viongozi wa kiislamu walilaan kitendo kile, na hata yaliyotokea Majuzi hapo Nigeria, kikundi cha Boko Haram kimeteka Dada zetu, na waislamu kote duniani piah tulilaan vitendo vile kwa kuwa walitumia kivuli cha Uislamu kufanya vitendo vile viovu. Nawaweka huru wenzetu kuwa sisi sio Magaidi na wala hatuupendi ugaidi.
**************************************


Vikundi vikubwa vya kiislamu nchini Marekan vya ISNA na CAIR vimekuwa mstari wa mbele kabisa kupinga vitendo vya ISIS ambavyo vinajenga uhasama baina ya Watu dunian. Vikundi hivyo viwili nchin humo vilisema kuwa, matendo hayo ni kinyume kabisa cha Uislamu, na uislamu haufundishi Ugaidi ila wao wana Maslahi yao mengine.
**************************************

Hata kule Uingereza pia zaidi ya wasuni na Washiite 100 walijiunga barabaran na kubeba mabango yaliyokuwa yakipinga matukio ya Kigaidi yanayofanywa na ISIS. Kiongozi wa Falme za kiarabu nae amelaani vitendo hivyo, kiongozi wa Uturuki na Indonesia nao wameonesha kutokukubaliana na kikundi Hicho kinachotumia Mwamvuli wa Uislam kufanya ugaidi.
**************************************

Kituo kimoja cha Zogby nchini marekani kimesema hata idadi ya Uislam imepungua kwa kasi kubwa kutokana na chuki dhidi yao. Watu wa Marekani wamekuwa wakiwachukulia waislam kama magaidi hali inayofanya waishi kama waliotengwa hivyo wengine wao wamehama uislamu, kutokea asilimia 36 ya mwaka 2010 mpaka sasa ni asilimia 27 tu. Kituo hicho kilisema, vyombo vya habari viomengeza kuonesha kuwa Uislam ni mbaya, hasa pale picha mbalimbali zinapoonesha matukio mabaya ya kigaidi na kuyahusisha na uislam.
****************************

Jambo la kumshukuru Mungu ni hapa nchini kwetu, tumekuwa na Ndoa kati ya dini zote kubwa mbili, tumekuwa familia moja, tukiishi kwa upendo bila chuki. Hatupaswi kuvunja familia yetu hii, kwa kudanganywa na nchi za Magharibi au video au picha zinazoonesha kuwa Uislam ni uigaidi. Ugaidi sio Dini bali ni vita vya kimaslahi. Sote ni Wana wa Mungu aliye hai, Mungu wa Adam na Hawa.


No comments

Powered by Blogger.