CHADEMA WANIJIBU HILI SWALI

Kuna watu wanasema CCM haijafanya chochote kwa miaka 54. Ni sawa tu. Ila je, somo la Civics
linafundishaje? CCM ilianzishwa 1961 au 1977?

¤Kama inazungumziwa tokea TANU basi ni kuanzia 1954 (kwa hiyo miaka 61). Kama ni CCM basi ni kuanzia 1977 (miaka 38). Kama ni kuanzia mfumo wa vyama vingi (mwaka 1992) basi ni miaka 23. Kama ni tokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi (1995) basi ni miaka 20.

¤Bila kujali ni 61, 54, 38, 23 au 20 kuna maswali magumu ma-3 (kama HARD TALK ya BBC enzi za Tim Sebastian)

1. Lowassa na Sumaye (walio UKAWA hivi sasa) walikuwa mawaziri wakuu kwa jumla ya miaka 13. Je, muda ambao CCM haijafanya lolote inajumuisha hiyo miaka 13?

2. Lowassa si anasema alisimamia shule za kata, kuvunja mkataba wa City Water, kuvuta maji Kahama kutoka Ziwa Victoria na ujenzi wa UDOM. Je, alisimamia akiwa chini ya chama gani? APPT Maendeleo?

3. Vyama vyote vikubwa na maarufu zaidi nchini vinatumia jina na sauti ya Mwalimu Nyerere kwenye matangazo yao ya audio na mabango. Miaka hiyo ambayo CCM haijafanya lolote je, inajumuisha miaka 23 ambayo Mwalimu Nyerere
alikuwepo madarakani kama rais
(1961/1962-1985)? Je, inajumuisha pia miaka mi-5 ya ziada ambayo Mwalimu Nyerere aliendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM (1985-1990)?

No comments

Powered by Blogger.