DE GEA KUONGEZA MKATABA, RONALDO ANA THAMANI YA BUGGAT, JAMES AUMIA

privaldinho.blogspot.com

Madrid Spain. Na Priva Abiud

Florentino Perez ameielezea PSG kuwa kama wanamtaka Cristiano Ronaldo basi wajiandae na Euro Billion moja. Mchezaji huyo Mwenye Miaka 30 msimu huu alihitajika na PSG kwa ada ya Euro 150 million, lakini Gazeti la El Mundo Deportivo lilisema kuwa madrid walikataa Ofa hiyo. Perez ameongeza kuwa" mkataba wa Ronaldo unaonesha kuwa Thaman yake ni Euro 1000 million ambayo ni sawa na Paundi 725 kama hawatofika ada hiyo basi wasahau kuhusu Ronaldo labda watafute Mreno au Mbrazili anaeitwa jina hilo sio huyu wetu".
***************************************
Alisema Pia, kuwa Ronaldo amebakiza misimu mitatu tu pale Bernabeu lakin akatilia mkazo kuwa ni "vigumu madrid kubaki bila mshambuliaji, haingii akilini kumuuza mchezaji wetu Bora kabisa kisa pesa za hao wafaransi, binafsi nampenda Messi lakini namhitaji zaidi Ronaldo kwenye timu yangu"
***************************************


USAJILI WA DEGEA

Perez amekiri kuwa kumpata De gea msimu huu hasa mwezi january haitowezekana maana mchezaji huyo yupo tayari kusaini mkataba Mpya Old trafford. Madrid ambayo ilitenga kiasi cha Euro 30 ili kumnasa De Gea msimu huu usajili huo ulikwama dakika za Mwisho kabisa. Alipoulizwa kuhusu kumpata De Gea katika dirisha dogo bure alisema kuwa "ni ngumu sana kumpata Mchezaji bora kiasi kile bure" mchezaji huyo Mwenye miaka 24 inaonekana kuwa yupo mbioni kuongeza mkataba wake ambao umebaki mwaka mmoja tu kuisha. Del Bosque ambaye ni kocha mkuu wa Hispania amemweleza De Gea kuwa kama hatokua chaguo namba moja kwenye klabu yake basi asahau kuitwa Euro 2016.


JAMES APATA MAJERAHA

Pigo lingine Madrid ni baada ya kuumia kiungo wao mahiri kabisa James Rodriguez alipokuwa katika mechi ya kirafiki akiwa na nchi yake dhidi Peru. Dokta wa Colombia bwana carlos Uloa amesema kuwa jeraha hilo sio kubwa sana. Madrid hawajasema kuwa atakaa nje kwa kipindi gani ila wamesema watasikiliza ushauri wa Madaktari wa hospitali Ya Universiatirio Sanitas La Moraleja.


No comments

Powered by Blogger.