KITABU CHA GERRARD
Chikoti Cico > SportSpapeR
YALIYOMO KWENYE KITABU CHA GERRARD, MY STORY
GERRARD AMZUNGUMZIA COUTINHO NA KAZI ALIYOPEWA NA SUAREZ:
-“Hakikisha unamchunga vizuri Coutinho” Hayo yalikuwa ni maneno ya Luis Suarez kwa Steven Gerrard wakati Suarez anaondoka Liverpool kwenda Barcelona, lakini pamoja na maneno hayo maneno mazito na jukumu Gerrad alilopewa nahodha huyo wa Liver kuna jambo linampa wasiwasi kuhusu Coutinho, kwenye kitabu chake anasema, lakini najua kwamba wababe wa Hispania, Barcelona na Real Madrid watakuja kumtafuta Philippe kwenye misimu michache kama walivyofanya kwa Luis, na hapo ndipo itakuwa ni jaribu kwa Liverpool kwasababu kutakiwa na moja ya klabu hizo mbili ni jambo zito kwa mchezaji yeyote kutoka Amerika ya Kusini ama Hispania lakini mpaka hayo yatokee Liverpool wanatakiwa kumuenzi Philippe.
GERRARD NA NDOTO YA KUIFUNDISHA LIVERPOOL:
-Gerrard anaanza kwa kusema “haitakuwa jambo kushangaza kuifundisha Liverpool siku moja?”,. Kwasasa sijui kama ntakuwa vizuri vya kutosha ama hata ntaombwa kufanya kazi hiyo hapo baadaye” mosi na cha kwanza kabisalazima nijiskie mjasiri kwamba naweza kuwa Meneja mwenye mafanikio, kamwe sitachukua kazi kupitia mgongo wa jina langu ama kwasababu tu baadhi ya mashabiki watapenda mimi kuwa kocha kwa msingi wa kwamba waliniunga mkono wakati nikiwa mchezaji”.
-………kama ntakuwa Meneja siku moja najua nitakaopenda awe masaidizi wangu, Xabi Alonso ama Jamie Carragher, ni waerevu na wana taaluma ya kina kuhusu soka na ni watu wa pekee, kama nikizungukwa na watu makini na Makocha sahihi nyuma yangu napenda kufikiri ntakuwa Meneja mwenye mafanikio”.
-Akiwa tayari amefanikiwa kupasi leseni daraja B la ukocha huku akisubiria kufanya leseni daraja A ya UEFA Gerrard anaendelea kusema “…. Nitapenda kutumia muda na makocha wachache
wakubwa, kivipi utashindwa kujifunza kama utapata nafasi ya kuzungumza kwa kina kuhusu utawala na Mourinho, Wenger, Hodgson na Rodgers? Hii ni pamoja na Pep Guadiola, natamani kutumia wiki moja kuangalia kazi ya Pep”
GERRAD NA KAZI YA KUSHAWISHI WACHEZAJI KUJIUNGA NA LIVER:
Moja ya majukumu ya Gerrard kama nahodha wa Liverpool ilikuwa ni kuwashawishi wachezaji mbalimbali ambao klabu yake iliwahitaji, hapa Gerrard anawazungumzia Willian na Kroos alivyojaribu kuwashawishi,
-…..2013, mchezaji tuliyemhitaji alikuwa Willian, nilifanya jambo la kawaida kila ninapowasiliana na mchezaji nyota tuliyetaka kumsajili, badala ya kumipigia simu moja kwa moja mara kwa mara nilituma sms, inaonekana ni heshima zaidi na inampa fursa mchezaji kusoma ujumbe wangu kwa muda unaomfaa zaidi, kupiga simu nilihisi sio sawa, niliwasiliana na Willian, niliongea nikitumai asingejiskia vibaya kwa mimi kuwasiliana nae moja kwa moja, nilimweleza ninavyomhusudu kama mchezaji……. Kama utahitaji kuchati ama kuuliza swali lolote nitapatikana kwa muda wowote”
-Baada ya Gerrard kujaribu kumshawishi Willian mara kwa mara mwishoni majibu yakawa hivi……… Ujumbe uliofata wa Willian ulikuwa wazi kabisa hata ningeweza kumwandikia kabla sijausoma, alisema “itakuwa vizuri sana kucheza timu moja nawe lakini sina hakika kama Liverpool itaweza
kunipa Ligi ya mabingwa (UCL), alikwenda Chelsea”.
-Mchezaji mwingine ambaye Gerrard alikuwa na kazi ya kumshawishi alikuwa ni Toni Kroos, anasema “lengo letu 2014 lilikuwa ni matumaini ya kipuuzi…… Brendan aliniomba nijaribu kuzungumza na Toni Kroos asajili Liverpool………
Nilijua Real Madrid walitaka kutuma ofa Bayern Munich na hivyo nlijiskia hovyo wakati namtumia sms".
-"Kroos alikuwa njiani kushinda kombe la Dunia kwa nchi yake na Real walikuwa mabingwa wa Ulaya lakini Mungu humpenda anayejaribu na hivyo nilijaribu. Baadhi ya wachezaji bora duniani wanaweza kuwa na heshima sana, Kroos hakunifanya nijiskie mjinga kabisa lakini ni kweli karibu atasaini kwa Real Madrid. Tulikuwa na mazungumzo mazuri ya sms na nilisema “vizuri na kila la kheri”.
Leave a Comment