BINGWA MTETEZI APIGWA 149-0

Madagascar Na Priva Abiud

Mnamo mwaka 2002 Shirika la Soka nchini Madagascar walimfungia kocha wa klabu Ya Stade Olyimpique De L'Emyrne (SOE) na wachezaji wanne wa klabu hiyo baada ya Timu hiyo kujifunga Magoli 149-0 dhidi ya As Adema na kuweka Rekodi ya dunia kwa magoli Mengi. Walijifunga magoli hayo kwenye Mechi ya klabu Bingwa oktoba Mwaka 2002.
********************
**************
*********
****

Chanzo kinasema kuwa ni wachezaji walilalamikia Maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo. Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo Bwana Jacques Benomy wa Malagasy Football Federation (FMF) alitoa hukumu kwa wachezaji wafuatao

1. Mlinda mlango ( Mamisoa Razafindrakoto ,pia nahodha ya timu ya taifa ijulikanayo kama The Scorpions aitwaye Manitranirina Andriananiaina na Mchezaji Mwingine ni Nicolas Rokotoarimanama na Domonique Rokotonandrasana wao walifunguiwa Mpaka mwisho wa Mwaka 2002

2. Wachezaji watimu zote walipewa Onyo kali

3 na Pia kocha wa SOE Zaka Be alifungiwa miaka mitatu kutokujihusisha na Mpira na pia asionekane kwenye kiwanja chochote cha soka.

Klabu hiyo ya SOE ndio walikuwa Mabingwa watetezi wa kombe hilo, waligomea maamuzi ya Refa, hata hivyo kombe hilo As Adema waliliitwa! Hata hivyo wizara ya Michezo nchini huko waliwafukuzisha kazi wafanyakazi wa FMF.

No comments

Powered by Blogger.