KWANINI NYERERE ALIMCHUKIA LOWASSA?
Mwl. Nyerere alikuwa ni kati ya
binadamu wachache sana wanaoweza kuyaangalia, kuyachambua na kuyatafakari mazingira ya wakati uliopo na kupata jibu mbadala la matokeo yake katika wakati ujao.
Maneno na ushauri wa Mwl. Nyerere uliwafanya baadhi ya watu ambao hawakumuelewa wapuuze lakini ukweli wake waliupata baada ya matokeo kuwafika. Watu wengine watajenga hoja na kusema, Mwl. Nyerere alikuwa na uwezo wa kutoa baraka au laana ya kisiasa kwa wale waliojishughurisha na kazi za kisiasa katika Taifa letu lakini mimi ninasema alikuwa ni kati ya watu waliokuwa na uwezo wa kupima hali ya kimazingira na kupata majibu sahihi au yaliyokaribu na usahihi.
Baadhi ya watu kama Mzee Mwinyi na Rais Kikwete waliokubali ushauri wa Mwl. Nyerere na matokeo yake yanafahamika kwa wale wanazifahamu siasa za Tanzania. Ni Mwl. Nyerere huyo huyo baada ya kuisoma Katiba ya CHADEMA akasema hiki ndicho chama kitakachokuwa mbadala wa CCM kwa maana kuwa, siku ambayo CCM itaondoka madarakani, basi itaondolewa na CHADEMA.
Your browser doesn't support the video tagNyerere akielezea namna walivyomkata lowassa
Kuna baadhi ya watu hawakuamini hasa ikichukuliwa kuwa kwa wakati huo, NCCR-Mageuzi ilikuwa ni chama maarufu na kikuu cha Upinzani.
Kwa sasa ninadhani ni mjinga au mpumbavu atakayekataa
ukweli uliobainishwa na Mwl. Nyerere. Wakati akiongea na Gazeti la Rais Mwema toleo la 371, Augustine Mrema alikaririwa akisema, “Nilikutana na Mwalimu kijijini kwake Butiama mwaka 1995. Aliniambia ‘Mrema, kwa nini unataka kuwania urais? Utaundaje Baraza la Mama Mawaziri? Achana na urais. Wania ubunge na mimi
nitakuja kukufanyia kampeni ili
ushinde’. Hata hivyo sikufuata
ushauri wake''.Kwa kutokufuata ushauri wa Mwl. Nyerere, hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa ndoto za Mrema katika mbio za Urais na hata umaarufu wake mkubwa wa kisiasa. Mwanasiasa mwingine ni Mzee Samwel Malecela ambaye alipewa ushauri na Mwl. Nyerere kupitia Kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania lakini kwa jeuri akaamua kuupuuzia. Matokeo yake yalidhihirika baada ya jina lake kushindwa kupita hata kwenye mchujo wa kwanza wa kumpata mgombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 na 2005. Kwa kukataa ushauri wa Mwl. Nyerere, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kifo cha kisiasa kwa Mzee Malecela. Kila mtu anafahamu yaliyotokea hata kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Mtera! Hatuwezi kuwa sahau wanasiasa wengine mashuhuri waliokaidi ushauri kama Oscar Kambona, Aboud Jumbe, Horace Kolimba n.k ambao maisha yao ya kisiasa yalifika ukingoni mapema bila wao kutegemea. Kwa sasa kuna jina la Edward Lowassa ambalo pia limeishapata ushauri wa Mwl. Nyerere mwaka 1995 wakati wa kutafuta mgombea Urais wa Tanzania.
Mwl. Nyerere alikaririwa ndani ya
kikao kikuu cha CCM akisema,
"Hapa hatuchagui mtu maarufu,
tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu.
Mwl. akimpongeza kikwete wakati wa uteuzi wa Rais Mwaka 1995
Kaauli ya Mwl.Nyerere ilichagizwa hivi karibuni na andiko aliyekuwa
Katibu( msaidizi mkuu kiserikali ) wa Mwl. J.K Nyerere, Mzee S. H. Kasori ambaye alimnukuu Mwl. Nyerere akisema, “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowassa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowassa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowassa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowassa asikose ubunge. Kweli Lowassa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashid ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowassa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu?’’.
Your browser doesn't support the video tagMwl hakupenda Viongozi Vigeugeu
Kuna uwezekano mkubwa kwa Mhe. Lowassa kutaka kuupuuza ushauri wa Mwl. Nyerere akidhani ana kundi la watu wengi nyuma yake kama alivyokuwa akidhani Augustine Mrema na kukaririwa na Gazeti la Raia Nwema akisema, “Nisingewania urais ningewakatisha tamaa mamilioni ya Watanzania waliokuwa wanataka Mrema awe Rais wa Tanzania. Kulikuwa na kauli mbiu maarufu wakati ule iliyokuwa ikisema Piga, ‘Ua Mrema Rais’.
Natumaini amejiandaa na matokeo
lakini kama hajafanya hivyo, Ingekuwa vizuri vile vile akajiandaa
kisaikologia na matokeo kama
yaliyowafika wale ambao walipuuza ushauri wa Mwl. Nyerere katika mtazamo wa kisiasa ndani ya siasa za Tanzania.
Kama Mhe. Lowassa ataamua kuliweka jina lake kwenye mchakato wa kumpata mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, inawezekana jina lake litashindwa hata kupita kwenye mchujo wa kwanza wa wagombea nafasi ya Urais na hata kama litapitishwa, siamini kama anaweza kushinda au kuwa Urais. Mwl. Nyerere ameondoka lakini ushauri wake bado unaishi katika mifano hai ya kisiasa nchini.
Na Mg'mpalala
imeandaliwa na Priva ABIUD
Posted via Blogaway

Leave a Comment