PACQUIAO KUGOMBEA URAISI
PACQUIAO KUGOMBEA URAISI.
Bukidnon, Ufilipino.
Na Priva Abiud
Manny Pacquiao ameliambia shirika Moja la habari nchini ufilipino kuwa amebakiza pambano zaidi ya Moja aachane na mchezo wa ngumi. Promoter Bob Arum, alisema kuwa Pac Man ataachana na ndondi 2017. Pac Man alisema kuwa, "ninajua kinachoendelea kwenye mwili wangu, siwezi kusubiri mpaka 2017"
********************************
Pac Man mwenye miaka 36, alisema hayo jumanne iliyopita, akitengua kauli ya Promoter wake huyo kutoka Marekani. Taarifa zinasema kuwa huenda pia akacheza pamoja kabla ya kurudi kuendelea na uchaguzi wa nchi yake, ili kuendelea na nafasi ya useneti. Manny Pacquiao alipata nafasi hiyo ya useneti mwaka 2010 mwezi wa tano, na akachaguliwa tena mwaka 2013,
***************************************
Hata hivyo Pac Man ambae ni kocha mkuu wa klabu ya kikapu ya Mahindra, isitoshe pia ana cheo katika jeshi, cheo cha Lieutenant colonel kwenye jeshi ya Ufilipino amesema kuwa umefika wakati wa kupumzika kutokana na mwili wake kuchoka. Bondia huyo aliyetoroka kwao na miaka 14 kutokana na Hali ngumu ya maisha amesema kuwa, amesema amekuwa akisumbuliwa na bega lake la kulia, amesema pia mwaka 2016 huenda akapigana pambano mwezi wa 4, lakini hajamtaja atakaekipiga nae.
**********************************
Mbali na kupoteza pambano kwa matokeo yaliyojaa maswali mengi dhidi ya mayweather kule Las Vegas miezi minne iliyopita hajasema kama atagombea cheo kikubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao. Taarifa zilijaa mitandaoni kuwa anataka kugombea Uraisi lakini hajazungumzia suala hilo kabisa! Ingawa Bob Arum ameongeza kuwa Mteja wake huyo huenda akagombea Urais mwaka 2022 au baadae ila kwa sasa ataendelea na Useneti.
Leave a Comment