RAISI JAKAYA KIKWETE AMTAJA MMILIKI WA RICHMOND
By Nuzulack Dausen na Anthony Kayanda,
Mwananchi
Tabora/Kigoma. Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.
Kikwete aliyasema hayo jana wakati
akiwaaga wananchi wa Kigoma
katika Uwanja wa Lake Tanganyika
na kumtaka Lissu amtaje mwenye
Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa
kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete. Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo
limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba
wawekezaji na mifuko ya kijamii
kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.
Kadhalika, Rais Kikwete alizindua
jengo la Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) pamoja na nyumba 36 za bei
nafuu zilizopo katika eneo la Mlole,
Kigoma Mjini
Richmond Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.
Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo
limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa
akisema yeye hakuhusika, bali
alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke
kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa
wakubwa.
Mgombea urais wa CCM, Dk John
Magufuli amekuwa akienda mbali
zaidi akisema akichaguliwa
ataanzisha mahakama maalumu ya
kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.
Leave a Comment