RAISI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UFISADI ULIOTOKEA
Guatemala
Na Sofia Menchu, Priva Abiud
Raisi wa Guatemala Otto Perez amejiuzulu kama Raisi wa nchi hiyo mara baada ya kutuhumiwa na Rushwa pamoja na Ufisadi. Na baada ya kujiuzulu kwake alifikishwa katika vyombo vya dola ili kujibu tuhuma zinazomkabili. Bunge ya Nchi hiyo limethibitisha kujiuzulu kwa raisi huyo kwenye kikao cha dharura mapema jumanne hii.
Hata hivyo makamu wa Raisi wa nchi hiyo Bwana Alejandro Maldonado amekaimu nafasi hiyo ili kumalizia kipindi cha miezi kadhaa kilichobakia kufikia uchaguzi mkuu nchini humo. Wiki kadhaa zilizopita Maelfu ya waandamaji walionekana katika mji mkuu wa nchi hiyo na viunga vyake wakimtaka Raisi huyo kuachia Madaraka mara moja.
Sherehe kubwa na furaha zilitapakaa mji mkuu, baada ya Mr Otto kuachia utawala wake. Mr otto alisema, "ninaheshimu mawazo ya wananchi wangu, sina shaka kabisa, na nitaenda kulikabili hili". mr otto mwenye miaka 64, alikanusha tuhuma hizo na atafikishwa tena Mahakamani leo hii kujibu tuhuma hizo.
Mwendesha mashtaka alimtuhumu Mr otto kwa kesi ya La Linea, baada ya kusikika kwenye simu akijadili; kuondoa Ushuru kwa wanaoingiza Bidhaa ndani ya nchi hiyo na kupokea kiasi fulani cha Pesa kuhalalisha Msamaha huo.
Mwanasheria Mmoja kwa jina la Juan Carlos Carrera mwenye miaka 38 alisema, "hatimaye Raisi aliyekubuhu rushwa kwenye historia ya nchi hii amekwenda" huku akibeba bendera ya Buluu na Nyeupe ya nchi hiyo kwenye gari lake akipiga honi ya gari lake kwa nguvu. Aliongeza kuwa, Haya ni Mapinduzi ya Wananchi, maana ameigawa Guatemala kwa kipindi kirefu"
Mr Otto alikuwa amevaa Suti nyeusi akiwa kwenye mahakama kuu nchini humo huku mwendesha Mashtaka huyo akicheza sauti ya simu iliyorekodiwa! Mwendesha mashtaka huyo akisaidiwa na Kitengo cha kupambana na rushwa Cha CICIG kilikuta zaidi ya simu 89,000 pamoja na email 6000 za raisi huyo.
TANZANIA MPOOOOO!!! MABADILIKO
Imeandikwa na Priva Abiud.
Leave a Comment