STEVEN GERRARD NI MBAGUZI WA WAAFRIKA
Dakar Senegal Priva Abiud
GERRARD HAPENDI WATU WEUSI
Wakati dunia ikipiga vita ubaguzi wa rangi, mwenzetu Gerrard yeye ndio kwanza anaelekea Kwenye Hardware kununua rangi ili kuzidisha ubaguzi wa rangi ambao unaelekea kupauka hasa hasa ligi kuu ya Uingereza. El hadji Diof amekua moja kati wa wachezaji weusi waliobaguliwa sana katika ligi ya nchini huko.
*****************************
*********************
***********
Msenegali huyo ambaye aliichezea liverpool mechi 55 na kufunga magoli matano amewaacha waingereza midomo wazi kwa kumtuhumu Steven Gerrard kuwa ndiye kiongozi wa Ubaguzi akifuatiwa na John Terry wa chelsea. Matamshi haya yanakuja baada ya Steven Gerrard kuieleza dunia kuwa Diof hana faida yoyote kwenye soka! Binafsi najiuliza sana Gerrard alimaanisha nini, maana huyu ameichezea timu yake ya Taifa mechi 69 na kufunga magoli 21, hivi ni kweli hana faida kwenye soka?
**********************************
Cha ajabu huyu Diof ndio yule aliyetajwa kwenye ALL STARS ya kombe la dunia mwaka 2002 kule korea je hana faida? Huyu si yule mchezaji aliyetajwa kwenye wachezaji Bora 125 bora dunian akiwa namba 100? Huyu si ndiye yule waingereza wanaofanya kazi BBC walimpa tuzo ya mchezaji bora kutoka afrika mwaka 2002? Huyu si ndiyo yule mchezaji bora wa Afrika mwaka 2001 na 2002? Sasa inakuwaje unasema mchezaji bora kama huyu hana faida? Sasa kati ya Diof na Lambert nani mwenye faida?
***************************************
Lakini baadae Gerrard alifika mbali kidogo pale aliposema kuwa Ni Heri balotelli aliisaidia liverpool kuliko huyu Mwafrika! Gerrard Sasa haya ni matusi ya wazi! Sioni sababu hiyo! Alisema, "sijawahi kupoteza muda wangu kumfuatilia au kumfikiria Diof, alikuja kupoteza muda hapa liverpool, hakuna alichofuata" "nadhani mliiona alichokifanya Baloteli, niliwahi kumwonya Diof kuwa EPL siyo ya watu Weusi labda tu uwe mzaliwa wa ulaya" diof aliilezea gazeti moja huko Senegal.
**************************************
"Kila mmoja anamjua Gerrard, nilimweleza Gerrard kuwa mimi ni mtu mweusi sio mzungu hivyo usinitishie" miaka yote niliyokuwa pale hakuwahi hata kuniangalia usoni" hawa waingereza ni wabaguzi sana, ndio maana nilimtemea mate yule mskochi kule celtic, wale waingereza hawakuangalia alichofanya yule mskochi walinipa adhabu ya mechi mbili na wakakata Mshahara wangu wa wiki mbili, Gerrard hakunitetea ila aliongeza chachu.
*****************************
Ila Diof alijigamba kuwa mambo ambayo amefanya au mafanikio mabayo amepata Diof Gerrard hajawahi kuyapata. Anasema "wataalam wa soka dunian wamenichaguliwa kuwa mmoja kati ya wachezaji bora wa karne, pia niliwahi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa saba kombe la dunia."Kila ninapotembea ndani na nje ya nchi naheshimika sana"
+++++++++++++
Diof kwa sasa yupo kwenye klabu ya malyasia ya Sabbah na mpaka sasa hakuna aliyejibu madai hayo ya Diof
Leave a Comment