BORA JIWE KULIKO VAN GAAL

HIVI VAN GAAL LILE DAFTARI HALIJAJAA? KAMA BADO BASI BORA JIWE KULIKO VAN GAAL..


Kama ningepewa bastola basi ningeanza na van gaal. Sitojali records zake, sitojali umaarufu wake... Wala sitaki kusikia kuwa eti ni mzoefu wa soka toka zaman. Hizo habari hazina faida yoyote kwa united kwa sasa! Huyu mzee amekuwa mzigo kwenye hii timu.

UBABE WA KIPUUZI
Huyu kocha amekuwa na maamuzi ya kijinga yasiyo na faida yoyote kimaslahi. Kwa mfano mdogo tu huyu kocha alifukuzwa Buyern Munichen baada ya kugoma kumsajili Manuel Neuer, aliwahi kuingia kwenye mgogoro mkubwa na zlatan ibrahimovic pale Ajax, pia aliingia kwenye sakata zito dhidi ya Rivaldo kitu kilichosababisha kumfukuza Rivaldo barcelona ambapo alijiunga na Inter na kubeba Uefa.

Alimkataa Neuer ambaye kwa sasa hakuna kipa kama yeye hapa duniani, kamkataa Di maria leo angalia shughuli yake PSG, kamkataa chicharito ambae kwa sasa ananga'ara! Usisahau mgogoro wake dhidi ya Requelme, achana na bifu lake na koeman, weka pemben ishu yake na hristo!


MALALAMIKO
Scholes amemlalamikia sana van gaal, juzi juzi Keane nae kaingia kwenye sakata la kumlalamikia lvg. Binafsi nmekuwa nikilalamikia tu mifumo yake ya kipuuzi kwa mfano!

Martial
Huyu bwana Mdogo ameonekana kuwa mzuri zaidi hasa akicheza kama mshambuliaji au namba 10. Martial alipokuwa Monaco sawa alicheza Winga lakini alikuwa na magoli 9 pekee kwa takriban michezo 40 hivi. Kumbe utagundua kuwa ana madhara zaidi akisimama mbele au nyuma ya rooney.
Tokea amemuweka winga hajafunga goli lolote lile...


Blind.
Huyu jamaa sijui ni libero, sweeper au CB?? Binafsi napendelea kumuona akicheza pembeni zaidi kuliko katikati kwa sababu, kwanza ni miujiza kumuweka beki wa kati anaetumia mguu wa kushoto pekee! Mguu wa kushoto ni mzuri zaidi kwenye maudambwidambwi na sio hard football... Kingine ni umbo la huyu jamaa,,, hawezi kuparangana na akina costa n.k. Ila akiwa pemben anakuwa huru zaidi hata kucheza wing back....

Depay, Rooney, rojo....
Afadhali kidogo Rojo anaweza kucheza mpira mgumu, n mrefu na ana umbo la kivita hivo ni rahisi kwake kucheza CB kuliko blind... Depay sina tatizo nae,,, nampa muda.. Akiendelea kuzomewa hivi hivi basi ipo siku atakuwa bora.... Rooney ni maajabu mengine ambayo lvg anajaribu kuyaonesha... Rooney yupo chini ya kiwango... Hana hadhi ya kuendelea kucheza dakika 90.. Amecheza misimu kumi kwenye ubora wake.. N muda wake wa kutokea benchi kwa sasa...


Kila siku lvg amekuwa akiandika sasa.... Sioni jipya... Mpira ule ule... Matokeo yale yale je kuna faida gani yeye kuendelea kuandika??? Mimi sio mwalimu wala sina utaalam wowote lakini MPIRA NI KUONA... Huhitaji degree kuona makosa! Hayo ni machache tu lakini van gaal hufai kuwa Carrington


No comments

Powered by Blogger.