MAGAIDI WAVAMIA MCHEZO WA UFARANSA NA UJERUMAN

MAGAIDI WAVAMIA MCHEZO WA UJERUMANI NA FRANCE

PARIS Na Priva ABIUD

Ufaransa imekumbwa na tukio la kigaidi tarehe 13/11/2015 kwenye ukumbi wa Bataclan Concert ambapo ripoti zinaonesha kuwa zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha baada ya kupigwa risasi na mabomu maeneo mbalimbali katika mji mkuu wa ufaransa, Paris na eneo la Stade de France ambako timu ya taifa ya Ufaransa ilikuwa ikicheza na Ujeruman huku ufaransa ikiongoza 2-0!

Ufaransa imetangaza hali ya hatari ambako ni kwa mara ya kwanza tokea Mwaka 1945! Raisi wa ufaransa alikuwa pia akiangalia mchezo huo wakati shambulizi hilo lilipotokea. Hili ni tukio la aina yake tokea Mwaka 1950 katika vita yake nchini algeria wakati Ufaransa ilipokuwa ikipambana na harakati za ugaidi (dhidi na ndan) ya Uislam hasa wakati wa mapinduzi ya Iran, na jihad nchin Afghanistan.

Raisi wa Ufaransa bwana Francois Holland hivi majuzi amepeleka Jeshi lake nchini Mali kupambana na Kikundi Cha kigaiidi cha Al Qaeda. Hivi karibuni Mwezi January magaidi walivamia nchini humo na kuua watu 12. Hata hivyo inasemekana kuwa mashambulizi hayo ni mwendelezo wa uhasama dhidi ya vitendo vya marekani dhidi ya uislamu. Hata hivyo tukio hili la stade de france linafanana na tukio lililotokea kwenye mbio za marathon za boston nchini Marekan.

Kwingineko kansela wa Ujeruman Angela Markel amelalamikiwa sana na kitendo cha kuruhusu mamilion ya wakimbizi kutoka Syria kuingia nchini humo baada ya Kabineti ya Ulaya kulazimisha nchi za ulaya kuruhusu wakimbizi hao kupewa hifadhi.

No comments

Powered by Blogger.