MAN UNITED YATIBUANA NA KIPA WAKE
MAN UNITED YATIBUANA NA KIPA WAKE!
Manchester.
Na Priva ABIUD
Manchester United imethibitisha kuwa wamevunja mkataba na kipa wake baada ya kushindwana kwenye baadhi ya vipengele vya mkataba huo!
Goli kipa huyo ambaye aliichezea Serbia kwenye kombe la dunia la wachezaji wa umri wa miaka 20 ajulikanae kama Milinkovic Savic ameamua kujiunga na klabu Poland ijulikanyo kama Lechia.
Milinkovic alikumbana na vikwazo vya kucheza ligi kuu Uingereza baada ya kukosa kibali cha kufanya kazi katika taifa hilo. Hata hivyo alitumia Muda Mwingi kufanya mazoezi pekee yake katika kiwanja cha Belgrade. Anasema "napenda kucheza Manchester ila nilikosa kibali, nahitaji kulinda kipaji changu kwa kucheza mara kwa mara"
"Tuliposhinda kombe la dunia la vijana nilijisikia fahari kubwa, kilichobaki ni kushinda kombe la dunia kabisa, nilitamani sana kucheza united, lakini sidhani kama ni bahati yangu kwa sasa labda hapo baadae"

Leave a Comment