MOURINHO KWENYE VITA YA UFALME
MOURINHO NI MFALME ALIYECHOKA
Na Priva Abiud
**********************************
Kwenye soka kuna laana, wachezaji wakiamua basi itabidi utafute uchochoro! Miaka ya zaman kama 1800 hivi, mkoani kilimanjaro wilaya ya Rombo alitokea baba mmoja ambaye alikuwa mfalme wa wakati ule! Kipindi kile rombo lilikuwa taifa, taifa hilo la Rombo lilikuwa likitawaliwa na taifa la vunjo liliongozwa na koo za kwamakundi, na marealle! Warombo waliteseka sana,..... TUTAENDELEA
+++++++++++++++++
Mourinho amekutana na wakati mgumu sana kwa msimu huu. Wengi wanasema kuwa sababu ni kumfukuza yule dokta. Naweza nkasema ni hoja lakin sio ya msingi sana! Kimsingi mpira ni biashara, kila mchezaji ana malengo yaKE binafs! Na malengo yao ni Uchumi na makombe! Kama mchezaji akipata haya anachohitaji ni kuhakikishiwa namba ya kudumu au nafasi! Msimu uliopita chelsea ilitwaa ubingwa, na wachezaji wake wana mishahara minono tu. Je kwanini wagome? Kwanini wasuse? Je kufukuzwa kwa dokta wao kuna waathiri nini?
::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
TUNAENDELEA
Baba yule mfalme alizaa kijana wake, na kijana yule alitegemewa kuwa mrithi wa utawala ule lakini ikumbukwe watu kutoka taifa la vunjo walikuwa wakipeleka mifugo yao kwa watu warombo wawafugie kisha baadae wawachukue! Mtoto wa mfalme huyu alikuwa mwenye umbo kubwa sana. Siku moja alimwambia baba yake kuwa kuanzia leo hii mifugo ya watu wa vunjo ni yetu. Watu wa vunjo waligoma na vita kubwa ilitokea lakini kutokana na ujasiri wake na umbo lake warombo walishinda vita ile.
@@@@@@@@@@@@@@@@@
Mourinho ni mtoto wa mfalme Abramovic amekuta timu ipo katika wakati mgumu, wachezaji wengi wametumika kama watumwa hasa safu ya ulinzi, alijaribu kumuondoa Cole, lakin ivanovic, terry, azpilicueta na cahil walikuwa hawana mbadala. Nadhan kitendo cha mourinho kumfukuza vicky kimekua kisingizio tu, ila ukwel utabaki kuwa chelsea defense imechokaa! hazard amekosa discipline kimchezo, mourinho haabudu wachezaji kabisa. Mtoto wa mfalme baada ya kushinda vita dhidi ya watu wa Vunjo baadae alivamia wamasai na kuwanyang'anya ng'ombe zao.. Mourinho nae baada ya kubeba ubingwa amesahau kuwa Hazard ndiye aliyembeba game 5 za mwisho. Ni wazi kuwa mou alijiona mfalme, alijiona yeye ndiye mwamuzi wa kila kitu lakini wachezaji wake muhimu wameshachoka kivita
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Nadhani Mourinho alipogundua ana umbo kubwa na anaheshimika na amewapiga watu wa vunjo kama (man cty, united na arsenal) amewashinda hao lakini kashindwa kuilinda familia yake, wachezaji wameanza dharau, hawamsikilizi, wengine wamechoka, wengine wanatafuta upeo wa kwenda madrid. Baada ya mtoto yule wa mfalme kuingia vitan na wamasai warombo wengi walipingana na maamuzi yale hawakupendezwa na kile alichofanya mtoto wa mfalme.. Na ndipo ubabe wa mtoto yule ukaanza kupungua kama wa Jose Mourinho. Pole sana Mou... Tafta mbinu ya kutatua migogoro ya ndan
Leave a Comment