MWANAMKE ALIYEPOTEA MIAKA KUMI APATAKINA AKICHEZA GAME

MWANAMKE ALIYEPOTEA MIAKA 10 AKUTWA AKICHEZA GAME!

QIANGIANG, CHINA.
Na Priva ABIUD

Mwanamke mmoja nchini china amepatikana kwenye chumba cha Internet akicheza game baada ya kupotea kwa muda wa miaka 10. Msichana huyo mwenye miaka 24 aliondoka nyumban kwao baada ya kugombana na wazazi wake mashariki mwa china katika Jimbo Zhejiang.


Mwanamke huyo ajulikanae kama Xiao Yun alisemekana kufa baada ya kupotea kwa muda wa Miaka 10 lakini mnamo tar 20 november mwaka huu alikutwa na Polisi akiwa katika chumba hicho alichotumia kucheza magame tokea akiwa na miaka 14.

Inasemekana alikuwa akitumia Kitambulisho feki ndipo polisi wa mtaa huo waligundua kuwa yule mwanamke alikuwa sio wa eneo hilo na walianza kumfanyia uchunguzi kabla hawajamfikisha kituo cha polisi na kutoa taarifa nyumbani kwao.

Polisi wanadai kuwa alikuwa akiishi kwenye maeneo ya kucheza magame na mara nyingi alilala kwenye mabafu mbalimbali. Hata wakati Mwingine aliaminika zaidi na wamiliki wa cafe na waliamua kumfanya msimamizi wa cafe hizo ili kujipatia pesa za kujikimu n.k

Mama yake mzazi aliumia sana na anadai kuwa tokea mwanae amepotea hajawahi kubadilisha namba kwa matumain kwamba ipo siku atampigia. Aliongeza kuwa "mimi ni mama mkorofi, nmekuwa nikimpiga na kumuonea sana Mwanangu Mara kwa Mara, kwa sasa amekuwa mtu mzima siwezi kufanya hivyo tena.


No comments

Powered by Blogger.