NDEGE YALIPULIWA NA BOMU

LONDON. Na Priva ABIUD

Shirika la upelelezi lililokuwa likichunguza ajali ya ndege ya Urusi limedai kuwa Ndege hiyo imelipuliwa na Bomu lililotegwa kwenye Ndege hiyo kabla ya kupaa.

Ndege hiyo aina ya Metrojet Airbus A321 ilipata ajali nchini Misri na shirika hilo limesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa kikundi cha ISIS kimehusika na ajali hiyo ambako ndege hiyo ilidondoka katika penisula ya Sinai


Hata hivyo shirika hilo limetoa tamko kuwa bado hawajatoa jibu lao la mwisho kuwa nan mhusika mkuu lakin taarifa zao za awali ni kuwa ndani ya ndege ile liliwekwa bomu ambalo lililipuka na kusababisha ajali.


Taarifa nyingine zinasema kuwa shirika la ndege la Shamr el-sheikh limesitisha safari zake za nchin Uingereza kwa hofu ya ugaidi. Zaidi ya Waingereza 20,000 wamekwama katika viwanja vya ndege kwa hofua ya kile kilichotokea!


No comments

Powered by Blogger.