REAL YAMTIMUA KOCHA WAKE

REAL YAMTIMUA KOCHA WAKE

Na Priva ABIUD
Real Sociedad wapo nafasi ya 16, na game mbili zijazo watakutana na Sevilla na Barcelona. Ni wazi kuwa hizi game Sociedad hawatatoka! Baada ya Moyes kushindwa kutimiza haja ya wana Man united mwezi wa nne 2014 walimfukuza kocha huyo na hatimaye alijiunga Real Sociedad baada ya miezi 10 ya tabu pale united.

Kocha huyu mwenye miaka 52, aliyetumia miaka 11 everton hatimaye ametimuliwa tena pale Real sociedad. Hii imekuja mara baada ya kuibeba Basque mpaka nafasi ya 12 msimu uliopita tokea mwezi wa 11 mwaka 2014. Real sociedad wamevunja mkataba wa moyes kwa kile kilichodaiwa kuwa kiwango kibovu, hata hivyo kocha msaididiz Billy Mckinlay nae ametimuliwa huku kocha msaidizi wa Barca bwana Eusebio Sacristan akichukua nafasi ya Moyes ambapo atakaa mpaka mwezi wa 6 2017.

Wasifu mdogo wa Moyes
Amezifundisha klabu za Preston (1998-2002) ambako alicheza mechi 234 na alishinda michezo 113 tu, everton 2002-2013 michezo 513-218 pia man united 2013-14 michezo 51 akashinda 27, sociedad 2014-15 michezo 42 amepata kushinda mara 12 tu.

Wapo watu wanasema kuwa hawamtaki van gaal bora arudi Moyes! Binafsi sijui wametumia vigezo vipi ila mimi sina shida wacha nyimbo iendelee ikiisha tutaweka nyingine

No comments

Powered by Blogger.