WAFUNGWA WATENGENEZA BASTOLA KWA SABUNI
WAFUNGWA WAKAMATWA KWA KUTENGENEZA BASTOLA:
Na Priva ABIUD.
Wafungwa wawili wanakumbwa na Mashtaka ya kutengeneza Bastola feki ili kujaribu kutengeneza mazingira ya kutoroka gerezani. Polisi wamesema mnamo siku ya Ijumaa Wafungwa hao walitengeneza Bastola hiyo kwa kutumia Sabuni na Toilet Paper katika Gereza la Lafourche Parish Detention Centre huko Louisiana.
++++++++++++
polisi hao wanadai kuwa mhusika mkuu ni Bwana Troy Benner ambaye alifungwa kwa makosa ya wizi wa kutumia mabavu na silaha, hata hivyo Mkuu wa Gereza alisema kuwa bwana Troy alimuibia askari magereza mmoja funguo ili kufanikisha mipango yao ya kukwepa kifungo chake.
+++++++++++++++
Wachunguzi walisema pia kuwa Bwana Troy alipanga kutumia silaha yake hiyo feki ili kuwatishia walinzi huku akisaidiana na Mwenzake Bwana Treiston Pierron ambaye alifungwa kwa makosa ya kuchoma nyumba. Watuhumiwa wote wawili wamefunguliwa kesi, huku Benner (49) alifunguliwa kesi ya kutaka kutoroka Gerezani na Mwenzake Pierron (32) akishtakiwa kwa kutaka kusaidia uhalifu.
Leave a Comment